Marquee

Pata habari za Jamii,Biashara,Burudani na michezo!!

tangazo

Tuesday, October 5, 2010

Zain yatangaza zawadi kabambe katika usajili wa simu


Zain yatangaza zawadi kabambe katika usajili wa simu

Dakika 30 za maongezi kutolewa kwa kila namba inayosajiliwa
Shilingi 100,000 kushindaniwa kila siku kwa kila mkoa


Dar es Salaam, Oktoba 05, 2010

Kampuni ya simu za mkononi ya Zain, ambayo ndio inayoongoza hapa nchini kwa kutoza viwango nafuu vya huduma za mawasiliano, leo imezindua promosheni yenye lengo la kuwazawadia dakika 30 za bure za muda wa maongezi wateja wanaosajili namba zao.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Mkurugenzi wa Huduma kwa wateja wa Zain, Irene Madeje Mlola amesema, kwa kila mteja atakayesajili namba yake, atajipatia muda wa bure wa maongeza wa dakika 30 ambazo ataweza kuzitumia kwa muda wa siku mbili na pia kila siku, shilingi laki moja zitashindaniwa na washindi kutoka mikoa yote nchini.

“Ni jambo la furaha sana kwetu pale tunapoona ya kwamba si tu kuwa mteja wa Zain anakuwa amejihakikishia namba yake kusajiliwa kabla ya muda uliowekwa wa zoezi hili, bali pia tunapoweza kumzawadia kwa hatua aliyochukua. Promosheni hii inalenga wateja ambao wamekuwa wakitumia namba za Zain lakini bado hawajazisajili”, alisema Mlola.

Ili kusajili namba, mteja anachotakiwa kufanya ni kutembelea ofisi za Zain au mawakala zaidi ya elfu sita waliosambaa nchi nzima, akiwa na nyaraka muhimu zinazomtambulisha. Wateja wote ambao hawajasajiliwa watapokea ujumbe wa SMS kila siku kutoka Zain kuwakumbusha kusajili namba zao na kuweza kujishindia zawadi hizi.

Nyaraka za msingi wakati wa usajili wa namba ya simu ni pamoja na kitambulisho cha kazi ama barua ya mwajili, Hati ya kusafiria, leseni ya udereva, kitambulisho cha kupigia ama barua inayotambulika na mamlaka husika za serikali.

Ili mteja anayesajili kadi yake ya Zain anaweza kuhakiki kama tayari amekwisha sajiliwa kwa kuandika *106#, kisha atapokea ujumbe mfupi wa maandishi ambao utaonyesha taarifa za mteja.

Katika kudhihirisha kujidhatiti katika kutoza viwango nafuu vya mawasiliano hapa nchini, pia hivi karibuni Zain ilipunguza kwa zaidi ya asilimia 50 katika gharama za kupiga simu kwenda mitandao mingine. Hadi kufikia sasa, Zain imekwisha sajili wateja takribani milioni nne na nushu, hii ikiwa ni karibia na asilimia 75 ya wateja wake wapatao milioni 5.9.
MWISHO


End
About Bharti Airtel Limited
Bharti Airtel Limited is a leading global telecommunications company with operations in 19 countries across Asia and Africa. The company offers mobile voice & data services, fixed line, high speed broadband, IPTV, DTH, turnkey telecom solutions for enterprises and national & international long distance services to carriers. Bharti Airtel has been ranked among the six best performing technology companies in the world by BusinessWeek. Bharti Airtel had over 188 million customers across its operations at the end of August 2010. To know more visit www.airtel.in

About Zain Tanzania
Zain is a leading telecommunications operator across the Middle East and Africa providing mobile voice and data services to 69.5 million active customers as at 30 June 2009. In terms of country footprint, Zain is the 3rd largest mobile operator in the world with a commercial presence in 24 countries.
Zain was voted the Most Respected Company in Tanzania for 2009 by top CEO’s through a survey conducted in East Africa by Nation Media Group and Price Waterhouse Coopers. Zain’s world class network covers all the regions of Tanzania thus allowing more individuals access to vital communication services. Zain was the first to introduce the Blackberry service in Tanzania. It also provides 3.5G, EDGE/GPRS services which allow customers to access to internet via their handsets and provides them with up-to-date global and local news, sports and entertainment.
Zain Tanzania is committed to supporting the community and environment it serves. Zain’s major community based project ‘Build. Our Nation’ will have provided over Tsh 870 million worth of teaching aids to schools throughout Tanzania by the end of 2010.

For More Enquires Contact
Muganyizi Mutta
Zain Tanzania Public Relations Manager - 0786 670 711

No comments:

Post a Comment

Related Posts Plugin for WordPress, Blogger...