Monday, November 15, 2010

KOCHA Fabio Capello ATANGAZA KIKOSI CHA ENGLAND



KOCHA Fabio Capello ametangaza kikosi kipya cha England ambacho kina mabadiliko kw aajili ya kujiandaa kwa mechi ya kirafiki dhidi ya Ufaransa kesho kutwa.

Mshambuliaji wa Cardiff City, Jay Bothroyd (28) amejumuishwa kwenye timu hiyo bila ya kutarajiwa, anacheza katika ligo daraja la kwanza.

Pia Christopher Smalling naye ameitwa akiwa ni mchezaji ambaye asota katika benchi la Manchester United.

Sura nyingine mpya katika timu hiyo ni mshambuliaji wa Newcastle United, Andrew Carroll na wa Sunderland, Jordan Henderson,lakini wachezaji hao watakuwa wakiangaliwa.

Capello ameeleza kwua anakusudia kuwatumia baadhi ya wachezaji wapya kwa mechi hiyo ya kirafiki ili kuweza kuweka mchnganyiko kwa ajili ya mechi za kuwani Euro 2010 baada ya mechi ya mwsho kutoka suluhu dhidi ya Montenegro.

Kikosi kamili cha England ni:

Makipa: Ben Foster (Birmingham), Joe Hart (Man City) na Robert Green (West Ham)

Walinzi: Kieran Gibbs (Arsenal), Ashley Cole (Chelsea), John Terry (Chelsea), Phil Jagielka (Everton), Joleon Lescott (Man City), Micah Richards (Man City), Rio Ferdinand (Man Utd) na Christopher Smalling (Man Utd)

Viungo: Theo Walcott (Arsenal), Jack Wilshere (Arsenal), Ashley Young (Aston Villa), Steven Gerrard (Liverpool), Gareth Barry (Man City), Adam Johnson (Man City), James Milner (Man City) na Jordan Henderson (Sunderland)

Washambuliaji: Gabriel Agbonlahor (Aston Villa), Jay Bothroyd (Cardiff), Andrew Carroll (Newcastle) na Peter Crouch (Tottenham)

No comments:

Post a Comment