Thursday, November 4, 2010

STARS KUFUNGUA NA ZAMBIA DESEMBA MICHUANO YA CECAFA


Katibu Mkuu wa Shirikisho la Vyama vya Mpira wa Miguu Afrika Mashariki na Kati SECAFA Bw. Nicolas Musonye akizungumza mbele ya waandishi wa habari leo kwenye Hoteli ya New Africa jijini Dar es salaam wakatim alipozungumzia maandalizi ya mashindano ya Tusker Challenge Cup 2010 yanayotarajiwa kuanza Novemba 27 hadi Disemba 11 mwaka huu. Akizungumza katika mkutano huo katibu mkuu huyo wa SECAFA Bw. Nicolas Musonye amesema timu 12 zimethibitisha kushiriki katika mashindano hayo ambazo ni Wenyeji Tanzania,Kenya, Burundi, Uganda, Somalia, Zanzibar, Ethiopia, Sudan, na ytimu zilizoalikwa ni Ivory Coast, Zambia na Malawi.
Mtendaji Mkuu wa SBL Bw. Richard Wells amesema SBL itahakikisha timu zote zinapewa huduma zote muhimu wakati zitakapokuwa hapa nchini kwa ajili ya mashindano ikiwa ni pamoja na Chakul, Mlazi na Usafiri wa ndege na itatoza zwadi kjwa washindi zinazofikia dola za Kimarekani elfu 60.000 ikiwa ni sehemu ya udhamini ambao ni dola za kimarekani laki 450.000 ambapo mshindi wa kwanza atajipatia dola 30.000, mshindi wa pili dola 20.000 huku mshindi wa tatu akijinyakulia dola 10.000. Kampuni ya Serengeti Breweriers ndiyo mdhamini mkuu wa mashindano ya Tusker Chalengfe Cup 2010 kwa mwaka huu.

No comments:

Post a Comment