Thursday, November 25, 2010

ZANTEL KUDHAMINI MASHINDANO YA GOFU GYMKHANA

Mkurugenzi wa Masoko wa Kampuni ya simu za Mikononi ya Zantel,Ikechukwu Kalu (kushoto) akizungumza na waandish wa habari wakati wa kutangaza kuzamini mashindano ya mchezo wa Golf ya wazi ya mwisho wa mwezi yatakayofanyika jumamosi Viwanja vya Gymcana Dar es Salaam.Wa kutoka kulia ni Ofisa Mkuu wa Masoko wa Zantel, Nitish Malik, Kaptani wa Golf, Joseph Tango na Mkuu wa mawasiliano wa Zantel, William Mpinga.

ZANTEL YADHAMINI MASHINDANO YA MCHEZO WA GOFU

Dar es Salaam, Novemba 24, 2010: Kampuni ya simu za mkononi ya Zantel imetangaza kudhamini mashindano ya mchezo wa gofu ya ya wazi ya mwisho wa mwezi yatakayofanyika Jumamosi ya wiki hii katika viwanja vya mchezo huo vya Gymkhana jijini Dar es Salaam.

Akiongea na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Afisa Mkuu wa Masoko wa Zantel Nitish Malik alisema kuwa Zantel imeamua kudhamini mashindano hayo ili kusaidia kukuza mchezo huo ili uweze kufahamika kwa watu wengi zaidi. “Gofu ni mojawapo ya michezo maarufu sana duniani kwahiyo nina imani kuwa udhamini wa Zantel katika mashindano haya utazidi kuutangaza huu mchezo zaidi na pia kupitia udhamini huu watu wengi wataweza kujitokeza zaidi kucheza mchezo huu’, alisema

Aliongeza kusema kuwa ana uhakika kwamba mwendelezo wa udhamini wa Zantel katika mchezo wa gofu utakuwa changamaoto kwa watu wengine kujifunza gofu na pia kupitia njia hiyo kuna uwezekano wa kupata wachezaji wazuri ambao hapo baadaye wanaweza kuiwakilisha Tanzania katika michezo ya kimataifa na kuiweka katika ramani ya kimataifa.

No comments:

Post a Comment