Sunday, December 5, 2010

Kampuni ya ALTAF yatoa msaada hospitali ya Mwananyamala


Kampuni ya ALTAF yatoa msaada hospitali ya Mwananyamala

Na Mwandishi Wetu

KAMPUNI ya ALTAF & COMPANY inayojihusisha na utengenezaji wa bidhaa za chuma, ya Pakistani yenye tawi hapa nchini imetoa msaada wa pesa na bidhaa mbalimbali kwa wagonja wa wodi zote za hospitali ya Mwananyamala vyenye thamani ya Sh. Milioni 1.5.

Katika msaada huo kampuni hiyo pia ilichangia damu salama lita tatu kupitia wafanyakazi wake kumi na mbili waliotembelea hospitali hiyo kuchangia wagonjwa waliopungukiwa damu.

Akizungumza mara baada ya kutoa msaada huo katika hospitalini hapo leo, Mkurugenzi Mkuu wa kampuni hiyo, Bw. Zulfqal Ali alisema kampuni yake imeguswa na kutoa msaada huo kutokana na mahitaji ya wagonjwa kuongezeka siku hadi siku.

"Wote tunaona wagonjwa hasa watoto wanaumia, na sisi tumeona tuungane na wenzetu kujumuika pamoja kusaidia sehemu ya jamii inayoteseka katika magonjwa ambayo yanaikabili jamii.," Alisema Zulfiqal.

Naye muuguzi katika wodi ya watoto hospitalini hapo Maina Erasmina aliishukuru kampuni hiyo na kuwaomba watu wengine kujitokeza kuisaidia jamii ili iweze kupambana na magonjwa kwa kuwa wahitaji bado ni wengi.

"Huu ni uamuzi mzuri na unaotia moyo kwa wagonjwa kama hawa kwa sababu wengi ni wahitaji sana tunaamini ujio wenu ni mwanga na wengine watafuaata.," alisema.

Mbali na damu, kampuni hiyo ilitoa bidhaa za Maji, Maziwa, Dawa za meno, Juice, matunda mbalimbali, pamoja na Sabuni za kuogea.

No comments:

Post a Comment