Wednesday, December 1, 2010

NDOVU SPECIAL MALT YAZINDUA KOPO LA DHAHABU LENYE UJAZO WA 330ML.


NDOVU SPECIAL MALT YAZINDUA KOPO LA DHAHABU LENYE UJAZO WA 330ML.

Dar es Salaam, Desemba 1, 2010: Kampuni ya bia nchini TBL kupitia bia yake ya Ndovu Special Malt leo imezindua kopo la dhahabu lenye ujazo wa 330ml. Kopo hili litapatikana sokoni pamoja na chupa ya kijani yenye foil ya dhahabu tunayoifahamu.

Akizungumza katika uzinduzi huo,meneja wa bia ya Ndovu Special Malt Oscar Shelukindo alisema kopo hili lenye muonekano wa kipekee unasherehekea bia ya Ndovu Special Malt kushinda tuza ya juu ya ubora ulimwenguni ijulikanayo kama Grand Gold Quality Award 2010 mwezi Mei katika International Monde Selection. “Hii ni Grand Gold ya kwanza kutunukiwa bia nchini Tanzania na tuzo hili hutolewa kwa bia yenye ubora wa asilimia 90 hadi 100 kwa ubora unaodhibitishwa na jopo la majaji wa kimataifa” alisema Shelukindo.

Kwa upande wake mpishi mkuu wa TBL Bwana Gaudence Mkolwe alisema “Ndovu Special Malt ndiyo bia pekee iliyotengenezwa kwa Crystal Malt,ambayo inaipatia bia ya Ndovu ladha nzuri ya kipekee zaidi”.

Alisema nia na madhumuni ya kuzinduliwa kwa bia ya Ndovu Special Malt katika muonekano wa kopo ni kuwapa wanywaji wa bia hii nafasi ya kufurahia ubora wa Ndovu bila usumbufu wa kurudisha chupa kwa kuwa Kopo ni rahisi kubeba,Ni la kisasa na linakupa Uhuru wa kufurahia Ndovu Special Malt wakati wote.

Nae meneja wa mawasiliano na habari wa TBL Bi Edith Mushi alisema Ndovu Special Malt inawajali wanywaji na itaendelea kuwaletea mambo mengi mazuri huku Ikitambuliwa kama bia yenye ubora zaidi nchini Tanzania.

No comments:

Post a Comment