Wednesday, December 8, 2010

usiku wa miller ndani ya kiota cha Sun Cirro leo usiku

Meneja Masoko wa TBL,Consolata Adam akionyesha moja ya kadi zitakazotumiwa na wageni watakaofika katika hafla hiyo ya usiku wa Miller hapo kesho katika klabu ya Sun Cirro iliopo Shekilango jijini Dar.
Meneja wa bia ya Miller,Victoria Kimaro (shoto) akizungumza mbele ya waandishi wa habari (hawapo pichani) kuhusu tamasha la usiku wa Miller linalotarajiwa kufanyika kesho katika klabu ya Sun Cirro,Shekilango jijini Dar.Kulia ni Meneja Masoko wa TBL,Consolata Adam

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha miller Guineone Fresh leo imetangaza rasmi kuwasili kwa kundi la Kode Reds Djs toka nchini Kenya kwaajili ya kutoa burudani kwenye usiku maalum wa familia ya Miller

Akizungumza na Waandishi wa Habari jijini Dar es salaam Meneja wa bia ya Miller Bi Victoria Kimaro alisema burudani hiyo itafanyika katika ukumbi wa club Sun Cirro uliopo Shekilango jijini Dar es salaam usiku wa jumatano ya Dec 08,2010 ambayo itakuwa usiku wa sikukuu ya kusherekea uhuru wa Tanganyika

Alisema usiku huo kutakuwa burudani za aina mbalimbali zitakazoongozwa na kundi zima la Kode reds Djs toka nchini Kenya ambapo kwa Tanzania mwanamuziki wa kizazi kipya Ambweni Yesaya “AY”atatoa burudani kwa kipindi chote

Kwa Upande wake TBL Brand Manager, Consolata Adam amesema maandalizi yote kwaajili ya tamasha hilo yamekamilika kwa kiwango kikubwa ikiwa ni pamoja na kuwawasili kwa kundi la Kode Reds Djs toka nchini Kenya“maandalizi yote kwaajili ya usiku wa miller yamekamilika kwa kiwango kikubwa na pamoja na burudani toka kwa kundi la Kod reds na AY lakini pia kutakuwa na DJs wa ndani ya Tanzania ambapo pia kutakuwa na burudani zenye ladha mchanganyiko zitakazowafanya watu watakaofika siku hiyo kukidhi mahitajio yao”

Alisema pamoja na wale watakaoingia ukumbini kwa utaratibu wa kawaida lakini kuna wanafamilia ya Miller waliopatiwa kadi maalum za mialiko wakati wa promosheni za miller hivyo kuwataka kujiandaa vilivyo kuhudhuria na kuwataka kukumbuka kufika ukumbini wakiwa na kadi zao.

Alisema lengo la Burudani hiyo ni kuweka utaratibu wa kuwakutanisha jamii nzima inayotumia kinywaji cha Miller na kukaa pamoja na kufurahi kwa pamoja kama wanafamilia”nawaomba wakazi wa Dar es Salaam na wapenda burudani kiujumla kuhudhuria kwa wingi pale Club Sun Cirro iliyopo Shekilango ili kwa pamoja tuweze kupata burudani na kufurahi kwa pamoja kwani aina ya burudani itakayokuwepo ni nadra sana kupatikana pahala pengine popote “alisema Bi Adam.

No comments:

Post a Comment