Tuesday, January 18, 2011

KESI YA JERRY MURO YASOGEZWA MBELE

Jerry Muro akiwa na mawakili katika
moja ya siku za kesi yake


Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu leo imeipiga kalenda kesi ya kula
njama na kuomba rushwa ya Sh milioni 10 kwa aliyekuwa mhasibu wa
Halmashauri ya Bagamoyo Michael Wage, inayomkabili mtangazaji wa TBC1,
Jerry Muro na wenzake Edmund Kapama na Deogratius Mgasa, hadi Januari
24, mwaka huu.

Hakimu Mkazi wa Mahakama hiyo Gabriel Mirumbe alifikia uamuzi huo
baada ya mashahidi wa upande wa mashtaka kutofika Mahakamani hapo.

Hakimu Mirumbe aliuonya upande wa mashtaka kuhakikisha wanawasilisha
mashahidi pindi shauri hilo linaposikilizwa kwani limechukua muda
mrefu bila kumalizika.

Kesi hiyo ilipoanza kusikilizwa Wakili wa Muro, Richard Rweyongeza
aliomba shauri hilo liahirishwe kwa kuwa Wakili wa mshtakiwa wa tatu
Majura Magafu hayupo.

Upande wa mashitaka ulikubaliana na upande wa utetezi ambapo Mwendesha
mashitaka Wakili wa Serikali Boniface Stanslaus, alidai hawakuwa na
mashahidi.

No comments:

Post a Comment