Monday, January 3, 2011

MAJINA MATATU YAINGIA FAINALI “TUZO YA SHUJAA WA SAFARI LAGER”.


MAJINA MATATU YAINGIA FAINALI

TUZO YA SHUJAA WA SAFARI LAGER”.


Dar es Salaam, Jumatatu 03, 2011: Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager na ushirikiano wa kituo cha ITV na Radio One, leo wameweka hadharani majina matatu yaliyofanikiwa kuingia fainali za tuzo ya “Shujaa wa Safari Lager”. Majina ya mashujaa hao ambao wanawania tuzo ya hiyo maalum ni:-

A. MERCY SHAYO – BOMANG’OMBE, KILIMANJARO

B. PAUL LUVINGA – SINZA E, DAR ES SALAAM

C. LEONARD MTEPA – MWANANYAMALA A, DAR ES SALAAM


Akitangaza majina hayo, Meneja wa Bia ya Safari Lager Fimbo Butallah alisema; “Tulipokea mapendekezo mengi toka kwa wananchi wakipendekeza mashujaa wao na mambo waliyofanya kwa jamii, kazi iliyofuata ilikuwa ni kupitia na kuchambua mapendekezo hayo kwa kuangalia vigezo muhimu, ili kuweza kupata majina matatu yatakayoingia fainali. Hatua inayofuata ni kuchapisha mambo waliyofanya mashujaa hawa watatu katika magazeti na kutangaza katika Televisheni na Redio ili wananchi wote waelewe na kisha waweze kupiga kura ili kuchagua shujaa wanaetaka atwae tuzo hii ya “Shujaa wa Safari Lager 2010”.

Tunapenda kuwakumbusha wananchi wote kuwa mshindi wa tuzo hii ya Shujaa wa Safari atajinyakulia kitita cha shilingi milioni 7, pia kutakuwa na shilingi milioni 3 ambazo zitasaidia shughuli yoyote ya kijamii atakayopendekeza shujaa huyo mahali anakotoka. Mashujaa wawili waliobaki wao watapata kifuta jasho cha shilingi milioni 1 kila mmoja.


Akielezea utaratibu wa kupiga kura; Mkurugenzi wa Redio One Bw. Deogratius Rweyunga alisema; “Baada ya kufuatilia mambo waliyofanya mashujaa hawa watatu walioingia fainali, wananchi watatakiwa kumpigia kura shujaa wanayetaka atwae tuzo hii ya “Shujaa wa Safari Lager”, line za kupiga kura zitakuwa wazi kuanzia leo hii hadi tarehe 21 Januari. Na jinsi ya kupiga kura ni kama ifuatavyo; Ingia katika sehemu ya ujumbe katika simu yako, andika neno Shujaa acha nafasi, andika herufi inayomwakilisha shujaa wako (A kwa Mercy Shayo,B kwa Paul Luvinga na C kwa Leonard Mtepa) kisha tuma kwenda namba 15310”. Utapata ujumbe kukuthibitishia kuwa kura yako imepokelewa.


Tuzo ya shujaa wa Safari Lager ilizinduliwa rasmi tarehe 24 Novemba 2010, ikiwa na lengo la kutambua na kuheshimu watu wanaofanya mambo makubwa yanayoleta mabadiliko kwa jamii inayowazunguka, bila kusukumwa na uwezo wa pesa wala madaraka waliyonayo.




-MWISHO-



Kwa Maelezo zaidi wasiliana na:

Fimbo Butallah, Safari Lager Brand Manager, +255767266567, fimbo.Buttallah@tz.sabmiller.com


Editha Mushi, Communications & Media Manager, +255767266420, editha.mushi@tz.sabmiller.com

Dorris Malulu, Public Affairs Administrator, +255767266049, doris.malulu@tz.sabmiller.com


Kuhusu TBL

Tanzania Breweries Limited (TBL) inatengeneza, kuuza na kusambaza bia, vinywaji vyenye ladha ya matunda vilivyo na kilevi na vinywaji visivyo na kilevi hapa Tanzania. TBL pia ndiyo kampuni mama ya Tanzania Distilleries Limited pamoja na kampuni shiriki ya Mountainside Farms Limited.


Bia zinazotengenezwa na kampuni ya TBL ni pamoja na Safari Lager, Kilimanjaro Premium Lager, Ndovu Special Malt, Castle Lager, Vinywaji vingine vinavyotengenezwa na kundi la makampuni ya TBL ni Konyagi Gin, Amarula Cream, Redd’s Premium Cold na Grand Malt.


Kundi la makampuni ya TBL limeorodheshwa kwenye Soko la Hisa la Dar es Salaam, limeajiri watu wapatao 1,300 na linawakilishwa nchi nzima na viwanda vinne vya bia, kiwanda kimoja cha kutoneshea, kimoja cha kutengenezea kimea pamoja na bohari nane za kusambazia bia.



No comments:

Post a Comment