Sunday, January 23, 2011

Super D kocha mwenye matarajio ya kuwafikisha vijana mbali katika ngumi


Awaomba wadau kushirikiana nae kuwasaidia vijana
MICHEZO hasa mchezo wa ngumi ni miongoni mwa michezo wenye msukumo mkubwa ukiwa umewapatia vijana nafasi ya kuwavutia katika jamii hasa katika kpindi hiki ambapo jamii zinajihusisha kwa karibu na michezo.

Ipo michezo katika jamii hasa hapa nchini ambayo imepokelewa kwa kiwango cha hali ya juu na mingine ikiwa bado haijapatiwa nafasi kubwa kama ambavyo inaonekana.

Mfano wa michezo ambayo imepta nafasi kubwa ya kupendwa na watu wengi hapa nchini ni mchezo wa mpira wa miguu, mchezo wa ngumi, na mchezo wa mchezo wa kikapu ingawa takwimu zinaoneshwa kuwa m,chezo wa kikapu ni wa pili kupendwa hapa nchini.

Ukiachilia mbali michezo hii ipo michezo mingine ambayo bado haijapewa nafasi kubwa katika maeneo mengi kwa mfano mchezo wa kriketi, gofu, mchezo wa meza, mpira wa mikono, tenisi na mingine mingi.

Wadau wengi wa michezo hapa nchini wamekuwa wakijihusisha karibu na michezo lakini wanashindwa kusonga mbele kutokana na msukumo wa jamii katika michezo kuwa mdogo inayopelekea kukosa wadau kudhamini michezo.

Kocha wa kujitegemea wa ngumi anayefundisha klabu ya Ashati ya Ilala Jijini Dar es Salaam Rajabu Mhamila 'Super D' ameanzisha programu maalumu ya kuwafundisha vijana anayoiendesha katika ufukwe wa bahari ya Hindi, sehemu ya Coco Beach.

Akizungumza na mwandishi wa makala hii hivi karibuni jijini Dar es Salaam Super D alisema alisema ameamua kuanzisha ili kutumia vizuri kipaji chake alichopewa na wengine waweze kufaidika nacho nao waweze kufaidika nacho.

"Nimeona vijana wengi hawana kazi wapo tu mitaani na wanavipaji sasa nafundishwa kwa kujitolea ili kuibua vipaji vyao na hatimaye waweze kutimiza malengo yao katika maisha.," alisema Super D kocha wa ambaye aliwahi kuchezea klabu ya zamani ya ngumi ya Simba Boxing Jijini Dar es Salaa.

Super D ambaye kitaaluma ni mwandishi wa Habari na mpiga picha wa Magazeti ya Majira, Spoti Starehe, Maisha, Dar Leo na Business Times yanayochapishwa na Kampuni ya Business Times ya Jijini Dar es Salaam anasema anaamini vijana wengi wanaweze kufika mbali kupitia mchezo huu kama wakiwezeshwa.

Anasema alianza programu yake ya ufukweni mapema mwezi Mei mwaka huu na kufanikiwa kupata vijana wachache lakini idadi yao hivi sasa imeongezeka hadi kufikia nane.

Kocha huyo anasema inawezekana pengine vijana wana vipaji katika ngumi lakini hawajui sehemu ya kupata mafunzo hivyo anawakaribisha vijana wengi kuhudhuri katika maeneo hayo kila siku za jumamosi na jumapili.
Anasema alianza programu yake ya ufukweni mapema mwezi Mei mwaka huu na kufanikiwa kupata vijana wachache lakini idadi yao hivi sasa imeongezeka hadi kufikia nane.

Kocha huyo anasema inawezekana pengine vijana wana vipaji katika ngumi lakini hawajui sehemu ya kupata mafunzo hivyo anawakaribisha vijana wengi kuhudhuri katika maeneo hayo kila siku za jumamosi na jumapili.
Anasema mabondia aliokuwa nao hadi hadi sasa wanafuatilia kwa makini mafunzo yake ambapo wengi wao wameonekana kuonesha nia na mapenzi ya dhati na mchezo huo.

"Sina shaka nao hata kidogo wanafanya vizuri na nawapongeza wanafuatlilia kwa makini na wananielewa viwango vyao vinazidi kubadilika kila kukicha wananipa moyo na nadhani watatimiza lengo.," anasema.

Akizungumzia mafanikio yake hadi amefanikiwa kuwa kocha Super D anasema alianza kujihusisha na mchezo wa ngumi mwaka 1984 na kujipatia uzoefu mkubwa baada ya kuchezea klabu mbalimbali za mchezo huo jijini Dar es Salaam.
Anasema klabu alizowahi kuchezea ni pamoja na klabu ya zamani ya Boxing iliyokuwa chini ya klabu ya soka ya Simba mwaka 1984, klabu ya reli iliyokuwa inamilikiwa na mamlaka ya reli kariakoo, pamoja na klabu ya Amana ya Ilala zote za Dar es Salaam.


Super D anasema akiwa bondia alipata nafasi ya kucheza na mabondia mbalimbali akiwemo Mbwana Matumla, Rashid Ally, Husein Pazzi, Alfred Ngaloma na bondia Roja Mtagwa ambaye ndiye bondia aliwewahi kumshinda kati ya hao ambaye kwa sasa anacheza ngumi nchini Marekani.
Alisema mabondia wengine aliowahi kucheza nao ni Oscar Manyuka, na Said Chaku ambaye kwa sasa ni mwamuzi wa mchezo huo katika mashindano mbalimbali yanayofanyika hapa nchini.
Hata hivyo hivi karibuni baada ya matunda ya kazi yake kuanza kuonekana kutokana na watu wengi kupendelea kupita na kutazama kazi yake baadhi ya wadau wameanza kujitokeza na kumpongeza.

Hata hivyo kocha huyo anasema anawaomba wadau wa mchezo huo wataungana naye kimsapoti ili kuwaendeleza vijana kutokana na ukosefu wa vifaa unaowakabili na wengi wao kushindwa kuhudhulia.

Anasema baada ya kuanza kazi yake hadi sasa amefanikiwa kumpata mdau mmoja aliyemtaja kwa jina la Zulfiqal Ali ambaye ameweza kumsapoti kwa kumpatia vifaa vyenye thamani ya zaidi ya Shilingi laki tatu.

"Ninamshukuru sana na nina mpongeza kwa kitendo chake cha kiungwana kuniunga mkono kuwasaidia vijana, nafikiri mfano wake utaigwa na wadau wengine namhakikishia ataifurahia kazi yangu,." anasema kocha huyo.

Hata hivyo kocha huyo amewataka wadau wengine kumuunga mkono katika kazi yake ambapo pia amewaomba wazazi kuwaruhusu vijana wao ambao wanavipaji kuhudhulia mazoezi yake ili kuendeleza vipaji vyao.

No comments:

Post a Comment