Monday, January 31, 2011

WAREMBO WANAOWANIA KISURA WA TANZANIA WAINGIA KAMBINI

WAREMBO wanaowania taji la Kisura wa Tanzania 2010/11, wameingia kambini leo katika Hoteli ya Kiromo View Resort, iliyopo nje kidogo ya Mji wa Bagamoyo,Pwani, tayari kwa fainali zitakazofanyika Machi 12, mwaka huu. Kambi hiyo itahusisha wasichana 25 kutoka mikoa mbalimbali nchini, waliofanikiwakutinga katika hatua ya fainali za shindano hilo, baada ya mchujo uliofanyika kwa miezi miwili.

Mchakato wa kuwapata wasichana
hao, ulianza Desemba 11, mwaka jana, na kumalizika mapema mwezi wa kwanza, ukihusisha warembo kutoka mikoa ya Mwanza,Mara, Kagera, Shinyanga, Tabora, Dar es Salaam, Arusha, Manyara, Dodoma, Iringa,Mbeya na Ruvuma.

Akizungumza wakati wa kuwatambulisha warembo hao katika Hoteli ya Kiromo ViewResort, Mwenyekiti na Mwanzilishi wa mradi wa Kisura wa Tanzania, Juliana Urio kutoka kampuni ya Beautiful Tanzanie Agency (BTA), alisema kuwa warembo walioingia kambini, ni wale waliopita katika mchujo baada ya kukidhi vigezovinavyotakiwa.

Vigezo hivyo urefu wa sentimita174, mapaja 36, kiuno 25, kifua 36 na umri ni kati ya miaka 18-27, bila kujali kama mshiriki ameolewa, kuzaa au la.“Mwaka huu idadi ya warembo walioingia kambini imeongezeka, kutoka 20 kama ilivyokuwa awali hadi 25, hii ikitokana na mdhamini wetu Kiromo View Resort kutupa nafasi ya pekee ya kuongeza wasichana watano zaidi,” alisema.Urio aliwataja warembo walioingia kambini kuwa ni Neema Methew na Silipa Swai kutoka Mwanza, Lilian Bussa na Gaudencia Joseph (Mara), Beatrice James (Kagera),

Monica Fikiri na Angella Mombeki (Tabora).Wengine ni Suzana Manoko, Winnfrida Sabega, Rita Swai, Lethina Christoper, Joyce Joseph, Happiness Salimenya, Grace David (Dar es salaam), Dotinata Soro, Neema Kilango, Neema Seley (Arusha), Kipoyane Laibon (Manyara), Mariam-Kissa Isaack, Asha Hamisi, Flavian Makungwa, Lucy John (Dodoma) na Queen Kabisama (Ruvuma).

Alisema kuwa wakiwa kambini, warembo hao watapewa mafunzo mbalimbali kuhusiana na maisha yao binafsi na jinsi ya kukabiliana na changamoto zinazowazunguka katika maisha yao ya kila siku, ikiwa ni pamoja na kutembelea maeneo tofauti. Urio aliwapongeza warembo waliopata bahati ya kutinga fainali za shindano hilo,ikiwa ni pamoja na kuwashukuru wazazi waliowaruhusu watoto wao kujiunga shindano hilo, akiwaahidi ‘kuwapika’ vilivyo warembo hao ili waweze kuwa mfano wa kuigwa kwa jamii ya kitanzania kutokana na matendo yao.

Mdhamini mkuu wa shindano hilo ambalo linafanyika kwa mara ya tatu sasa, ni Family Health International (FHI), wakati wadhamini wengine ni TBC1, Kiromo View Resort, TanFoam (Arusha), SBC Limited, Flare Magazine, Hugo Domingo, BASATA, GRM Production, Clouds FM, ATCL na MJ Records.

1 comment: