Sunday, February 13, 2011

‘SHOGA ’ AIBU KWA TAIFA ,BASATA TOENI TAMKO


TASWIRA YA COVER YA FILAMU YA SHOGA .
Na Shaban Matutu
LEO katika Vunjavunja tutakuwa na mada inayohusu uigizwaji wa filamu ya shoga.
Nianze kwa kuweka wazi kwamba nimekuwa na ndoto ya muda mrefu ya kuona tasnia ya filamu inakuwa na kuvuka mipaka ili waigizaji wetu waitangaze Tanzania kama nchi nyingine za Nigeria na Ghana (Nollywood), India (Bollywood), Marekani (Hollywood).
Chimbuko la ndoto hii ni uwepo wa mamluki wasiokuwa na uwezo wa kubuni hadithi zenye mvuto na za kufikirika zikiwa na uwezo wa kupenya katika soko la kimataifa.
Moja kati ya filamu ambazo zimenifanya kuandika makala hii ikiwa imeonyesha ufinyu wa kufikiri ni ya Shoga.
Pamoja na kupata matangazo ya kutosha kwa kumdhalilisha mwanaume lakini nadiriki kusema mwandishi wake yawezekana hakufikiri kwa kina au hakutafuta ushauri au pengine aliowapelekea wamshauri uwezo wao ulikuwa ni wa chini kuliko wake.
Filamu hii ambayo imeigizwa na msanii Tino, ambaye amekuwa kwenye tasnia hii kwa muda mrefu sasa imekiuka miiko na tamaduni za nchi yetu.
Nimeamua kulisema hili kwa sababu kuu nne; Kwanza, imenikera kuona mtoto wa kiume kudhalilishwa, pili mafunzo yake hayafuati maadili ya Tanzania, tatu kukiokoa kizazi chetu ambacho kimekuwa mstari wa mbele kuzitazama katika majumba yetu na wakati mwingine kwenye majumba ya starehe, nne ni aibu kwa wasanii wenzake walio katika tasnia hiyo.
Filamu hii kwa haraka inatoa somo ambalo sitaki kuliamin sana la kuwa na shaka na uwezo binafsi wa kufikiri wa Tino kuigizaji ushoga haijalishi kama filamu hiyo ataonekana akifanya kitendo hicho au la.
Tino kama kioo cha jamii kinachotazamwa na vizazi vyetu vijavyo atakuwa anawafundisha nini vijana wadogo kama mwanangu mpendwa Jumanne (3) baada ya kuiangalia filamu hii.
Tusije kushangaa kuona watoto wetu wakashindwa kucheza tena michezo yao kwa baba kuwa wa kiume na wa kike mama na badala yake tukawakuta wakicheza wanaume tupu mtu na shoga yake.
Ingawa sihitaji tufike huko lakini filamu hii inaweza kutufikisha kutokana na watoto kunasa mambo katika umri wao.
Tino kama mkongwe alitakiwa kuona mbali zaidi uliko kutazama mambo ya wazo jipya la kuigiza kama ya shoga maarufu kama Punga, Bwabwa, Gumegume na mengine ya aina hiyo katika nchi ambayo hatujafikiria hata siku moja kutangaza hadharani kuhusu kutambua haki za wapenzi ya jinsia moja.
Baada ya kumsikia kwa mara ya kwanza Tino akielezea uamuzi wake wa kutengeneza filamu hii ambayo ningependa kuiita ya kishenzi na inayotaka kuturudisha enzi za Sodoma na Gomora katika kipindi hiki kwa haraka niligundua lile jipu la waigizaji kujifanya wanaweza kila kitu katika utengenezaji wa filamu limepasuka.
Filamu hii imepita kiwango hata cha zile za Magharibi ambao labda kutokana na kutambua kwao haki za mashoga wangeweza kuigiza lakini wao hawajafikia kufanya hivyo.
Hapa nikabaki na maswali ambayo nilikosa majibu je ni kweli tatizo ni umasikini wa kutaka kuingiza filamu nyingi sokoni ili kujiingizia fedha kwa mawazo ya haraka? Au Tatizo ni waigizaji kujitia kuweza kila kazi katioka tasnia hiyo? Au ni uwezo wao finyu wa kufikiri unaochangiwa na kutokuwa na elimu ya kutosha ya sanaa wakibaki kutegemea sanaa pekee?
Niliendelea kujiuliza inawezekana kuna mtu aliyemlaghai Tino kwa nia ya kujiongezea umaarufu kwa kupitia njia ya mkato? Au nia yake ilikuwa kujitangaza kimataifa kwa kuwa ndiko wanatambua haki za mashoga? Au Tino anataka kudai haki za Ushoga kwa kupitia filamu yake hiyo?
Kama Tino wakati anaigiza alikuwa amejiuliza swali kati ya hayo hapo juu bila ya kutulia na kufikiri sawa sawa ajue amelitia aibu Taifa ambalo lina mambo kibao ya kuyaigizia na kupeleka nje na kuuzika kama vile vifo vya waandamanaji w a Pemba, Arusha na matatizo ya kuingia mikataba feki iliyosababisha waziri Mkuu kujiuzulu.
Tino alipoifanya maskini wa Mungu akili yake ilimtuma ni mali yake bila ya kujua kuwa kila anachokifanya kama Mtanzania kikiwa cha aibu basi atakuwa ameliingiza taifa katika aibu hiyo.
Filamu kama hiyo ingetengenezwa nchi za Uingereza, Marekani na nyingine zinazotambua haki za kishoga kwangu isingekuwa neno lakini kutokana na tendo lenyewe hata waigizaji kama
Steven Siegel, Rambo, Jet Lee, Danzel Washington, Jackie Chan hawajawahi kuigiza filamu yenye mlengo huo pamoja na mashoga kuandamana kila siku.
Ningependa kumshauri Tino kama alikuwa anataka kuomba haki za usho ga asingetumia sanaa angeomba
Kwa njia nyingine kama alivyofanya Elton John ambaye pamoja na ushoga wake hajawahi kuimba wimbo wa kuomba haki hiyo kama mwanaume.
Filamu kama hii inapopenya kwenda kwenye soko la kimataifa inajenga taswira chanya miongoni mwa wale wanaoiona ambako watanzania watatafsiriwa kama moja ya nchi zinazotangaza utamaduni wa Sodoma na Gomora.
Shoga imepambanua ufinyu wa shule za sanaa walionazo wasanii wa hap a nyumbani kwa kuonyesha kuwa uwezo wao wa kufikiri ni mdogo sirahisi mtu mwenye akili isiyokuwa ya mwendawazimu kuigiza shoga na kupita barabarani kifua mbele bila wasiwasi.
Hili ni funzo kubwa kwa wasanii wetu kuona umuhimu wa kwenda shule ya sanaa ili waweze kuwa wabunifu kila kukicha kwani msanii anayekuwa amekwenda shule si rahisi kufifia mapema.
Mara kadhaa msanii Baba Haji amekuwa akisema kuwa siku zijazo tutacha
mbua yupi msanii wa kweli na yupi mbambaishaji kwa hili nimeweza kumgundua mbambaishaji ni yupi.
Nini cha kufanya? Kwa sababu bado filamu hii haijauzika sokoni ni jukumu la Wizara ya Habari na Utamaduni kwa kupitia Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) kuhakikisha filamu hii inapigwa marufuku kabla ya kusambaa na kufikia watu wengi.
Iwapo watapuuza tahadhari ninayoitoa ni kutegemea kupata taifa lenya akina Tino wengi zaidi majumbani mwenu.
Basata kama chombo kinachojihusisha na masuala ya sanaa kinatakiwa kulitazama hili kwa jicho la tatu kama vile wanavyokuwa wakipigia kelele uvaaji hovyo wa wanamuziki na kufungia kwa baadhi ya nyimbo za waamuziki wanapoona zimekosa maadili.
Hili lisiishie hapo inatakiwa sasa Basata iunde chombo kitakachosimamia ukaguzi wa filamu kabla ya kuingia sokoni kiholela kama inavyofanyika hivi sasa.
Natoa angalizo iwapo tutawaacha hawa wenye akili za Tino tusijekushangaa kuona filamu za ngono kwa kisingizio eti msanii hachagui nafasi ya kuigiza hata kama inapingana na utamaduni au imani ya dini zote mbili.
Basata kwa hili mkilifumbia macho pindi tutakapozalisha kizazi cha mashoga hapo baadaye dhambi hiyo na iwatafune kwani kazi yangu nimeikamilisha.
Mungu atubariki kwa kutuepushia usodoma na ugomola huu.

http://bongoweekend.blogspot.com/

No comments:

Post a Comment