Thursday, March 24, 2011
KAMPUNI YA SIMU YA ZANTEL YAPUNGUZA GHARAMA
KAMPUNI ya simu za mkononi ya Zantel wametambulisha viwango vipya vya kupiga simu vijulikanavyo kama ‘Umoja Tariff’ kuthibitisha viwango vyake ni bora na vya gharama nafuu sokoni. Viwango vya Umoja vinamwezesha mteja wa Zantel kupiga simu kwenda mitandao mingine kwa TSH 2.50 kwa sekunde ikilinganishwa na TSH 3 kwa sekunde ya mitandao mingine. Pia wateja wa Zantel watafaidika zaidi na viwango hivi vya Umoja kwa kupiga simu kwa robo shilingi (TSH 0.25) Zantel kwenda Zantel kila siku kuanzia saa 5 usiku hadi saa 2 asubuhi.
Kaimu Meneja Masoko wa Zantel Bw.Brian Karokola,akizungumza na waandishi wa habari, alisema viwango hivi vipya alisema “Zantel inaheshimika kwa ubunifu na viwango na huduma zake zinazotumikia kila sehemu ya soko. Tunafahamu kuwa wateja wetu wanapendelea nini na kupitia viwango vya Umoja tumewapa wanachotaka ambacho ni thamani inayowawezesha kuongea kwa muda mrefu kwa gharama ndogo.” Viwango vya Umoja ni kwa wateja wa Dar es Salaam na Zanzibar pekee.
Wiki iliyopita Zantel walizinduwa viwango vipya vijulikanavyo kama Twanga Zaidi kwa wateja wake wa mikoani vinavyowawezesha wateja kupiga simu kwa robo shilingi Zantel kwenda Zantel masaa 24 na TSH 1.99 kwa sekunde kwenda mitandao mingine.
“Mtandao wa Zantel unajali wateja wake na kupitia viwango vyetu vipya tunakidhi mahitaji yao ambayo ni kuwawezesha kuwasiliana muda wowote kwa gharama nafuu na bila masharti.” Alimalizia Bw. Karokola.
No comments:
Post a Comment