Thursday, March 10, 2011

MAISHA YAKIMAPENZI


Pia, kama mwanaume ameishi na mwanawake kwa muda mrefu na amekuwa na desturi ya kufanya mepenzi mara kwa mara katika mazingira yale yale anaweza kukumbwa na kasoro hiyo. Hivyo anashauriwa kubadili mazingira ya kufanyia mapenzi, kupeana mahaba mapya, kuamsha mapenzi kwa kujaliana, pia kuondoa fikra zote zenye kukinaisha ikiwa sambamba na kuzingatia usafi wa mwili. Yakifanyika hayo mwili utaitikia taarifa ya akili na nguvu zitapatikana.

Kwa wanaoshindwa kurudia tendo wanatakiwa kufuata kanuni hizo hapo juu. Jambo kubwa ni suala la kuuzoeza mwili. Usiulazimishe kuanza mara moja kwenda mara nyingi wakati mapenzi yako yamekuwa ya kuiba mpaka baba alale na wakati mwingine muda wako wa kutoka kazini umebana na hivyo kukufanya ufanye mapenzi ya chap chap kila siku. Ukiwa mtu wa namna hii haiwezi ikatokea siku moja ghafla tu ukafanya mapenzi mara tatu bila kuchoka.

Pia inawezekana mwanaume akashindwa kurudia tendo si kwa sababu hana nguvu bali hapewi ushirikiano wa kutosha toka kwa mpenzi wake. Hivyo wakati wa kutafuta uwezo wa kwenda raundi nyingi ni vema usaidizi wa mwanamke ukatolewa, isitokee kupokea lawama tu za “huwezi, sijatosheka” kwani hizo ndizo zinazowafanya wanaume washindwe kabisa kwa hofu kuwa wanaaibika. Mawazo ya kuaibika yanapopewa kipaumbele huufanya uume kuzidi kusinyaa, kwa maana hiyo ni vema kuyatupilia mbali na kuacha kujihukumu.

Pia kuna hitilafu ya wakati wa kuridhishana, inaweza kutokea mwanamke akawa kamaliza raundi yake ya kwanza, wakati anaingia msisimko wa pili mwanaume anafika kileleni, kinachotokea ni mwanamke kumlazimisha mwanaume arudie tendo kwa muda mfupi tangu amalize, jambo ambalo ni vigumu. Sasa ikitokea mwanaume kachezewa na hana msisimko anapata hofu kuwa hawezi, ikijengeka hivyo hata iweje jambo hilo halitawezekana tena. Hivyo ni bora kupeana muda wa kupumzika kabla ya hatua ya pili ya mchezo.

Pale inapotokea hamasa ya kurudia haipo fikra za mwanaume zisipewe nafasi ya kushindwa kwani nyakati, mchoko, makujukumu, hofu za maisha na mambo kama hayo yanapokuja katika siku ya kustarehe ni wazi kuwa kiwango cha ufanyaji mapenzi kitakuwa chini na hali hii huwatokea wanaume wote, hata walio hodari wa kwenda raundi kumi kwa siku.

Sambamba na hilo wanawake wanashauriwa kutoonesha kujali pindi inapotokea hali hiyo, badala yake wawaambie wenzao kuwa siku hiyo inatosha hata kama hawajatosheka, lengo ni kuondoa hofu ambayo ndiyo msingi wa wanaume kuishiwa uwezo wa kufanya mapenzi. Hata hivyo maudhi, kufanya mapenzi na usiyempenda, msongo wa mawazo na kutokuaminiana huchangia kupoteza msisimko wa kuwa ‘kidume’.

Ushauri wangu ni kwamba chochote ambacho unataka mwili wako ukifanye lazima uuzoeze. Ukizoea kuamka saa 12 asubuhi mwili utatii kanuni hiyo. Na ukizoea kufanya mapenzi kila siku mara mbili au tatu hali itakuwa hivyo. Mwisho katika sura hii ni vema wanaume na wanawake wakajifahamu kuwa uwezo wa kufanya mapezni unapungua kufuatana na umri, isitokee mtu akakosa raha kisa hawezi kwenda mara nyingi kama zamani wakati anajua kabisa umri wake umekuwa mkubwa.

Jamani kutafuta nguvu za ujana zirudie uzeeni ni kujipa taabu ya bure. Wakimbiaji hodari wa zamani leo hawezi kutimua mbio kama ilivyokuwa enzi za ujana wao! Ikiwa tumeingia kwenye umri wa utu uzima lazima tufahamu kwamba mwili unaishiwa uwezo, hivyo ni vema tukakubaliana na hali. Lakini jambo la kushangaza siku hizi hata vikongwe wanapanga foleni kwa waganga kutafuta tiba ya kufanya mapenzi mara tatu kwa siku! Mapenzi yanataka uwezo wa akili na mwili tusishindane na uwezo asili tutapoteza muda na pesa bure.

Tatizo la mwisho ambalo nalo linatajwa kuwasumbua zaidi wanaume ni maumbile madogo ya uume. Wanaume wengi wamekuwa wakilalamika kuwa maumbile yao yanawazuia kuwapa dozi wapenzi wao. Lakini kama nilivyosema huko nyuma kwamba mapenzi hayana kanuni kwamba lazima mtu awe hivi ili amtosheleze mwenzake. Kinacholeta raha katika mapenzi ni hisia, hii ikiwa na maana kwamba mwanaume au mwanamke anaweza kufurahia mapenzi kwa kutomasana na kuhamasishana kwa viungo vingine vya mwili na kujikuta wameridhika hata bila ya kuingiliana.
Kwa maana hiyo wale ambao wanamaumbile madogo wanaweza kutafuta wanawake ambao nao wanamaumbile ya aina yao. Baadhi ya wataalamu wanasema kwamba kwa kawaida umbile la nyeti za mtu linakwenda sambamba na urefu wa mwili wake.

Kwa maana hiyo wanawake wafupi (si wote) wanatajwa kuwa na nyeti zinazolingana na maumbo yao. Hivyo wanaume wenye kasoro hii wanatakiwa kutafuta wanawake wenye maumbile madogo na zaidi wajifunze michezo ya kimapenzi. Kwa sababu za kimaadili ni vema wenye tatizo hili wakawasiliana nami.

Hitimisho la makala haya kwa ujumla. MOJA ni kuepuka hofu. Ikitokea siku moja umeshindwa katika tendo la ndoa haina maana una kasoro, bali ni hali ya kawaida, hivyo usifadhaike, utakuza tatizo. Kwa wale wenye tatizo hili wapunguze wasiwasi na wajiamini. PILI, nguvu za kiume zinahitaji mwili wenye nguvu, hivyo ni busara kula lishe bora na kufanya mazoezi yasiyokuwa makali sana. TATU, kumfundisha mwanamke namna ya kukusisimua. NNE, kuepuka mawazo ya kuhuzunisha wakati wa tendo. TANO, kupata muda wa kupumzisha mwili. SITA, kuepukana na pupa, tumia muda usiopungua dakika 20 kufanya romance. SABA, kujiamini.

No comments:

Post a Comment