Tuesday, March 22, 2011

wasanii wa five star waliopata ajali na kufariki na wale waliojeruhiwa watajwa

wasanii wa five star waliopata ajali na kufariki na wale waliojeruhiwa watajwawasanii wa five star waliopata ajali na kufariki na wale waliojeruhiwa watajwaBaadhi ya wasamalia wema waliokuwa kwenye foleni ya magari baada ya kutokea kwa ajili ya Basi ndogo la Wasanii wa Kundi la Five Stars Moden Taarab wakichunguza kwa makini iwapo kuna mtu aliyebanwa ama kusahauliwa kuokolewa ama miili wake kubakia eneo hilo baada ya basi hilo kuparamia lori lililosheheni mbao lililokuwa limeharibika njiani , katika barabara kuu ya Iringa- Morogoro , eneo la Hifadhi ya Taifa ya wanyama ya Mikumi, karibu na Kijiji cha Doma, Wilaya ya Mvomero usiku wa kuamkia leo.
Lori lililoparamiana na basi la wanamuziki wa Five Stars

wasanii wa five star waliopata ajali na kufariki na wale waliojeruhiwa watajwaMsanii wa kikundi cha Taarab cha East African Melody Bi Mwanahawa Ally ( 55) akiwa wodini katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro leo baada ya kujeruhiwa kwenye ajali ya basi dogo la wasanii wa Kundi la Five Stars Moden Taarab la Jijini Dar es Salaam. Yeye alikuwa msanii mwalikwa kwenye safari hiyo ya kikazi katika mikoa ya nyanda za juu kusini . Picha zote na habari na John Nditi wa Globu ya Jamii, Morogoro


Majina ya wanamuziki wa bendi ya Five Star Modern Taarab waliokufa katika ajali ya gari Mikumi mkoani Morogoro usiku wa kuamkia leo yamefahamika.

Kwa mujibu wa mkuu wa kikosi cha usalama barabarani mkoani Morogoro Be. Ibrahim Mwamakula, marehemu hao ni Issa Kijoti, Nasoro Madenge, Mapande, Fembe Juma, Omary Hashim, Tizo ,Omari Tall,Ngeleza Hasan,Hamisa Omari,Maimuna 'Kisosi', Haji Msaniwa na mcheza show wa kundi la Kitu Tigo Ilala

“ Hii ajali imepoteza watu 13 kati ya hao 12 wamefariki papo hapo na mmoja
amefariki akiwa anapatiwa matibabu Hospitalini.

"Ni ajali mbaya kutokea iliyohusisha magari matatu, ambapo waliokufa wote ni kutoka kwenye basi dogo la wasanii wa kikundi cha Five Stars na kusababisha majeruhu tisa kulazwa” alisema Mwamakula, akifafanua kuwa kati ya waliokufa 10 ni wanaume na watatu ni wanawake.

Amesema majeruhi tisa ambao wote ni wasanii waliolazwa katika Hospitali ya Mkoa wa
Morogoro ni pamoja na Mwanahawaa Ally( 55) kutoka Kundi la East African
Melody, ambaye alikuwa ni msanii mwalikwa, Susana Benedict(32), Zena Mohamed
(27), Samila Rajab (22)na Mwanahawa Hamisi (36)ambao wamelazwa wodi namba
tatu.

Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Kikosi cha Usalama Barabarani aliwataja
wasanii wengine waliolazwa katika Hospitali hiyo ni pamoja na Ally Juma
(25), Rajabu Kondo ( 25), Issa Hamis , Shaaban Hamis (41) na Msafiri Musa
(22).

Kwa mujibu wa Kamanda huyo wa Kikosi cha Usalama Barabarani Mkoa wa Morogoro, kuwa dereva huyo aliligonga lori hiyo wakati akijaribu kulikwepa Lori jingine lililokuwa likotokea mbele yake lenye namba T 530 BHY lenye tela T 182 BKB aina ya Scania ambapo katika harakati hizo basi hilo lililigonga Lori hiyo mbele pembezoni na kusababisha magari hayo kuanguka.

Alisema kuwa baada ya kuliparamia Lori hiyo , basi hilo liliyumba na kuhama uoande wake na kujibamiza kwenye Lori lililokuwa mbele yake ambalo halikuwa na mzingo kitendo kilichofanya paa la basi hilo kukatwa wa juu ambapo watu 12 waliokuwa ndani ya basi ndogo hilo kufariki dunia papo hapo na wengine saba kujeruhiwa vibaya .

Hata hivyo alisema , majeruhiwa mmoja kati ya saba alifariki dunia wakati alipokuwa akipatiwa matibabu katika Hospitali ya Mkoa wa Morogoro alipofikishwa kutoka eneo la tukio na kutambuliwa na ndugu zake kuwa ni Haji Mzaniwa ( 38), mwimbaji wa kikundi hicho.

1 comment:

  1. Nawapa pole ndugu ze2 wario pata ajari mungu awaraze maari pema yote kazi ya mungu

    ReplyDelete