Thursday, April 7, 2011

Airtel yazindua mnara wa mawasiliano Samunge kwa babu loliondo







KAMPUNI ya mawasiliano ya simu za mkononi ya Airtel, leo imetangaza kuzidi kupanua mtandao wake kwa kuzindiua huduma ya mawasiliano katika eneo la Samunge na maeneo jirani, wilayani Ngorongoro, mkoani Arusha.


Kwa mujibu wa Airtel Tanzania, kuzinduliwa kwa mtandao imara na wenye nguvu umegharimu zaidi ya dola za kimarekani laki moja na nusu hadi ulipomalizika. Uwekezaji huu utawezesha kuleta mawasiliano thabiti kwa watu wa vijiji vya Samunge, Mgongo, Mageri, Yasimdito and Digodigo.

Mkurugenzi Mkuu wa Airtel, Bw.Sam Elangalloor alisema Airtel imejidhatiti katika kutoa huduma bora na nafuu kwa watu wa Samunge, huduma inayoambatana na uwepo wa mtandao madhubuti pamoja na huduma nyingine zimekuwa zikipatikana.


Alisema mpango huo ni ahadi yake ya kuleta mawasiliano nafuu na yenye kuwafikia watanzania wengi zaidi, hasa walioko maeneo ya vijijini hapa nchini,



“Uwepo wetu wetu Samunge na maeneo mengine ya jirani, kwa hakika kutaleta chachu ya maendeleo ya kijamii na kiuchumi kwa wakazi na wageni wa maeneo haya. Kuwaunganisha watu wa Loliondo wakati huu ambapo mahitaji ya mawasiliano ni makubwa, kunadhihirisha dhamira yetu ya kuwa mbele zaidi kwa kila tunalofanya”, alieleza zaidi.


Alisema eneo la Samunge limeonyesha kuwepo ongezeko kubwa la wageni wanaotembelea, kutoka Afrika ya Mashariki na Kati, wengi wao wakiwa wanaelekea kupata tiba maarufu ya kikombe cha Mchungaji Mstaafu Ambikile Mwaisapile.


Alisema idadi ya wageni wanaoingia na kutoka kwa siku inakadiriwa watu 25,000 , huku eneo hilo likiwa linakabiliwa na uhaba mkubwa wa kutokuwa na mawasiliano ya simu za mkononi.

No comments:

Post a Comment