Monday, April 18, 2011

MKUTANO WA SIKU MBILI WA UWEKEZAJI AFRIKA WAANZA LEO DAR


Rais Jakaya Kikwete akitoa hotuba yake katika Mkutano wa Uwekezaji Afrika, leo katika ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam.
Mkurugenzi Mtendaji wa Baraza la Biashara Jumuia ya Madola Dk. Mohan Kaul, akizungumza katika mkutano huo.
Mkurugenzi Mkuu wa Kituo cha Uwekezaji Injinia Emmanuel Ole Naiko, akizungumza katika mkutano huo.
RAIS wa Burundi Pierre Kurunziza ambaye ni Mwenyekiti wa wakuu wa Nchi za Afrika Mashariki, akifungua mkutano huo.
Washiriki wakiwa kwenye mkutano huo
OFISA Mwendeshaji Mkuu wa Kampuni ya Vodacom Tanzania, Dietlof Mare, akizungumzia mikakati ya kibishara ya kampuni yake katika mkutano huo.
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Hawa Ghasia, akipata maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Bishara wa Kampuni ya Maxcom Africa, Ahmed Salim, kuhusu huduma ya Max Malipo inavyoendeshwa na kampuni hiyo, Maxcom Africa pia waliweka banda lao kwenye ukumbi wa Mlimani City wakati wa mkutano huo.
WAFANYAKAZI wa Kampuni ya Simu za mkononi ya Vodacom Tanzania, wakiwa kwenye banda la kutoa huduma ya 'Kama kawaida' kwenye wakati wa mkutano wa Uwekezaji Afrika, jana kwenye Ukumbi wa Mlimani City, Dar es Salaam. Huduma hiyo ni ya kumwezesha mteja wa kampuni hiyo, kuendelea kutumia laini yake popote alipo Afrika Mashariki.
RAIS Jakaya Kikwete, Rais Yoweri Museven wa Uganda na Rais Mwai Kibaki wa Kenya, wakipita kwenye banda la huduma za benki ya KCB, ambalo ni moja ya mabanda ya maonyesho yaliyokuwepo wakati wa mkutano huo.
BAADHI ya washiriki wa mkutano huo, wakiwa kwenye banda la benki ya Eco wakati wa mkutano huo. chanzo ni www.chachandudaily.blogspot.com

No comments:

Post a Comment