Thursday, April 14, 2011

SBL YAIMWAGIA TASWA MIL 80/ KWA AJILI YA TUZO


Mwenyekiti wa TASWA ,Juma Pinto wapili kushoto akizungumza na waandishi wa habari hawapopichani ikiwa ni pamoja na kuwashukuru Kampuni ya Bia Serengeti SBL, kwa kuthamini mchango wa wanahabari na kutoa udhamini wa sh.mil.80/- huku akisisitiza kwa wanahabari kuwa tuzo hizo zitakuwa zenye ubora kushinda tuzo zingine zinazotolewa hivi sasa. Tuzo hizo zitatolewa katika michezo zaidi ya 15 inayochezwa na jinsia zote pia kutakuwa na zawadi kwa mshindi mmoja wa mwaka. Wakati huohuo Pinto ameongeza kwa kusema kuwa Wanahabari wamekuwa wakidharauliwa na baadhi ya watu ambao wamekuwa hawathamini mchango wao mkubwa hivyo ametoa wito wanahabari kuungana na kuwa kitu kimoja kwa kuwa umoja ni nguvu."Hatuna budi kuwashukuru SBL, kwa utu waliotuonyesha kwa sababu tulitembeza bakuli la kuomba msaada katika Kampuni nyingi zinazotutumia lakini hawa wametuthamini licha ya kuwa sisi bajeti yetu ilikuwa ni kiasi cha Sh.Mil. 160 kiasi hiki tulichopata na ahadi zingine zitatusogeza na kufanikisha hafla hii kubwa ya chama chetu.

Mkurugenzi wa Mawasiliano na Uhusiano Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), Teddy Hollo Mapunda akikabidhi mfano wa hundi yenye thamani ya shilingi milioni 80 kwa Mwenyekiti wa Chama Cha Waandishi wa Habari Tanzania (TASWA), Juma Pinto,wengine kutoka kuliwa kwa pinto ni Makamu Mwenyekiti TASWA, Maulid Kitenge, Meneja wa Mauzo SBL, Nandi Mwiyombela na Katibu wa TASWA ,Amir Mhando.Hafla ya makabidhiano imefanyika leo asubuhi katika hoteli ya Royal Palm Movenpick.

CHAMA cha Waandishi wa Habari za Michezo Tanzania (TASWA), kimeitangaza Kampuni ya Bia Serengeti (SBL), kuwa wadhamini wakuu wa hafla ya utoaji tuzo za mwanamichezo bora wa 2010.
Ili kuonyesha kwamba tuzo hizo zinakuwa tofauti na miaka iliyopita, kadhalika kuthamini hadhi ya waandishi wa habari za michezo na wanamichezo, SBL imetangaza udhamini wa Sh milioni 80.
Kiasi hicho cha udhamini, kilitangazwa jana na Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda mbele ya waandishi wa habari kwenye Ukumbi wa Kivukoni, ulioko hoteli ya kimataifa ya Royal Palm-Movenpik, Dar es Salaam.


Aidha hafla ya utoaji wa tuzo hizo umepangwa kufanyika Mei 6 katika hotelini hapo.

No comments:

Post a Comment