Tuesday, May 3, 2011
BAYPOT YADHAMINI SHEREHE ZA WALIMU MKOA WA PWANI
Na Victor Mkumbo, jijini
TAASISI ya Kifedha ya Bayport, inaendelea kukua kwa kutoa mikopo na ajira za kudumu Vijijini.
Akizungumza jijini, Meneja Uhusiano na Masoko wa Bayport, Ngula Cheyo amesema kuwa wameamua kujikita katika kutoa ajili kwa watu mbalimbali ili waweze kufikia malengo.
Amesema kuwa Bayport imedhamini Chama Cha Walimu Mkoa wa Pwani baada ya kutambua mchango ambao wafanyakazi hao wameotoa katika jamii.
Amesema kuwa dhumuni la Bayport ni pamoja na kubadilisha maisha ya watu wengi kupitia utoaji wa mikopo isiyokuwa na dhamana.
Amesema kuwa Kampuni hiyo pia ina mikakati ya kutafuta Vijana wenye vipaji katika kila tawi ambalo wamelifikia, ili kuwawezesha kimaendeleo wao pamoja na jamii waliyoizunguka.
Amesema kuwa Bayportm ilianzishwa mwaka 2006 na kwa kasi imekuwa taasisi inayoongoza katika utoaji mikopo kwa waajiriwa wa Tanzania ambapo mpaka sasa ina jumla ya matawi 50 nchi nzima.
Amesema kuwa udhamini huo waliutoa katika Sherehe za Siku ya Wafanyakazi walipotembelea katika Mkoa wa Pwani.
Safi sana mkuu kamua vitu, nakuaminia
ReplyDelete