Wednesday, May 18, 2011

KOCHA JULIO ASAKWA NA POLISI

Na Shakoor Jongo
Kocha wa Timu ya Taifa ya Vijana chini ya Miaka 23 (U-23), Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ (pichani)anasakwa na jeshi la polisi, akikabiliwa na tuhuma za kutoa lugha chafu na kuharibu mali ukweni.

Julio a.k.a Alberto Perreira, anasakwa na polisi wa Kituo cha Magomeni, Usalama, Dar es Salaam kwa nambari ya kitabu cha ripoti za jeshi hilo (Report Book ‘RB’) MAG/RB/8313/2011 KUHARIBU MALI.

Chanzo chetu kilipasha habari kuwa Julio alifanya fujo, kutoa lugha chafu na kuvunja mlango wa nyumba ya mama mkwe wake.

Mtoa habari huyo alisema, Julio alifanya tukio hilo Mei 14, 2011, Magomeni Mapipa, Mtaa wa Tosheka, Dar es Salaam.
“Siku hiyo kulikuwa na kikao cha kifamilia ambacho kiliamua kuwa Julio na mke wake anayeitwa Efu Magembe wahame nyumbani hapo kwa sababu tangu mwaka 2009 hawajalipa kodi.

“Unajua hizi nyumba ni za kifamilia na kila mtu anayekaa hapa basi ujue kuna kitu ambacho kinamfanya akae bure. Nyumba ni ya mama mkwe wa Julio lakini anatakiwa kulipa kodi.

Siku alipoambiwa ahame, akaja juu, akatukana watu na kuvunja mlango,” kilisema chanzo chetu.

Jitihada zetu za kumpata Julio hazikuzaa matunda, kwani muda wote simu yake ilikuwa ikiita bila kupokelewa.
chanzo ni http://www.globalpublishers.

No comments:

Post a Comment