Friday, May 6, 2011
MSONDO KUFANYA ONESHO LA ZOTE KALI DDC KARIAKOO JUMAPILI
BENDI kongwe ya muziki wa dansi nchini, Msondo Ngoma 'Baba ya Muziki' itafanya onesho liitwalo 'Zote Kali' linalolenga kukumbusha nyimbo zao za zamani Enzi ya kuitwa NUTA,JUWATA NA OTTU.
Onesho hilo ambalo Msondo itapiga karibu nyimbo zote za zamani litafanyika jumapili kwenye ngome ya mahasimu wao wakubwa Mlimani Park Ochestra 'SIKINDE' Ukumbi wa DDC Kariakoo, jijini Dar es salaam.
Msemaji wa Bendi hiyo RAjabu Mhamila 'SUPER D' alisema katika onesho hilo la 'Zote Kali' Msondo itapiga nyimbo zilizotamba enzi hizo za NUTA,JUWATA NA OTTU ikisindikizwa na kundi la taarabu la Coast Modern 'Watafiti wa Mipasho'
Alisema mbali na nyimbo za zamani, pia bendi yao itapiga nyimbo mpya zinazoandaliwa kwa ajili ya albamu yao ijayo.
Alizitaja baadhi ya nyimbo zitakazopigwa kuwa ni 'Fatuma' Kimwaga, Asha Mwana Sefu, Queen Kasse, Nimuokoe Nani,Demokrasia ya Mapenzi, Solemba 'Piga ua Talaka Utatoa na nyinginezo
'Ni onesho la kwanza Maalumu kwa msondo kukumbusha enzi zake, ambapo tutashilikiana na kundi mahilri la taarabu la Coast Morden linaloongozwa na Mkali, Omari Tego' alisema Super D.
Nyimbo mpya zitakazopigwa na pamoja na 'Suluhu' uliotungwa na Shabani Dede 'Mzee wa Loliondo' Dawa ya Deni Kulipa wa DJ Papa Upanga, Lipi Jema' Mjomba Kibene wa Eddo Sanga na kibao cha 'Nadhiri ya Mapenzi.
SUPER D, alisema Msondo imeamua kuwandalia mashabiki wake onesho hilo baada ya wiki mbili za kuwa nje ya Dar es salaam kabla na baada ya Pasaka.
No comments:
Post a Comment