Monday, May 9, 2011

TIMU YA NGUMI YA ASHANTI KWENDA KUONESHA UFUNDI WA NGUMI TABATA


LIGI ya kuhamasisha mchezo wa ngumi kwa mkoa wa Ilala inatarajia
kufanyika tena Mei 14 kati ya mabondia wa Ashanti boxing na Matibwa
ambapo ianatarajia kutimua vumbi, Tabata Segerea Dar es Salaam.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Kocha mkuu wa timu ya Ashanti, Rajabu
Mhamila 'Super D' ambaye pia ni mratibu wa ligi hizo mkoa wa Ilala
alisema ligi hiyo itakuwa ikifanyika maeneo tofauti ya mkoa huo ili
kuweza kuhakikisha inawafikia wakazi wote wa Ilala.

Alisema, lengo hasa likiwa ni kutaka kuwavuta vijana wengi kujiunga na
mchezo huo na kuepuka kukaa vijiweni huku wakiwa na kipaji cha kucheza
mchezo huo ambapo mapambano ya ligi hiyo yatakuwa katika raundi nne
katika uzito tofauti.

Alisema, katika mchezo huo wa hivi karibuni kwa upande wa klabu ya
Ashanti mabondia watakaoenda kuchuana na mabondia hao wa Tabata ni
Ibrahim clas atakae chuana katika uzito wa kg 60, Uwesu Manyota 58,
Ramadhani kimangala kg 56, Rashid Mhamila kg 54, Mack Edison kg 52 na
Musa Mohamed kg 49.

Alisema, kwa upande wa Ashanti wamejiandaa vizuri kiushindani kwani
mabondia hao wote wapo katika kiwango cha juu hivyo wanaimani
kuwaangusha mabondia wa klabu hiyo ambao ndio wenyeji wa mashindano
hayo.

Alisema Super D mbali ya kuamasisha mchezo wa ngumi pia kutakua na DVD
zilizoandaliwa na kocha uyo kwa ajili ya kujifunza sheria za mchezo
pamoja na jinsi ya kufanya mazoezi ambazo kuna mabingwa wa Dunia
akiwemo manny Paquao, Floyd Maywether, Oscar Dela Hoya,Mohamedi Ally
na wengine wengi

No comments:

Post a Comment