Mwakilishi wa Shirika la Makazi laUmoja wa Mataifa (UN HABITAT) Philimon Mutashibirwa akifungua semina siku moja kwa Vijana wasanii chipukizi kutoka wilaya za mkoa wa Dar es Salaam leo asubuhi katika ukumbi wa Karimjee jijini Dar es Salaa. Semina hiyo imeandaliwa na kituo cha Vijana cha UN Habitat cha jijini Dar es Salaam kwa lengo la kuwapa elimu vijana chipukizi wanaojishughulisha na sanaa za aina mbali mbali kutambua wajibu na haki zao katika kazi zao za sanaa kwa lengo la kuziboresha ili ziwaletee tija. Katika ufunguzi huo mgeni Rasmi Philimon Mutashibirwa aliwaasa vijana kuwa makini, kutia nia sambamba na kujiwekea malengo ya muda mfupi, wa kati na malengo ya muda mrefu ili waweze kufanikisha malengo yao. Kushoto ni Afisa Vijana Wilaya ya Temeke Anna Malika. Wa kwa kwanza kulia ni Afisa kutoka BASATA Omar Mayanga na wa pili kushoto ni Gadi Karugendo Mratibu wa Vijana kutoka Shirika la Makazi la Umoja wa Mataifa kituo cha Dar es Salaam. |
No comments:
Post a Comment