Wednesday, June 1, 2011

MSHIRIKI WA BIG BROTER MTANZANIA ANENA KINAGAUBAGA KILICHOMWONDOA MJENGONI


MSHIRIKI wa Tanzania katika shindano la Big Brother Amplified, Lotus, amesema kutolewa kwake katika shindano hilo ni sehemu ya mchezo.
Lotus alitolewa katika shindano hilo la sita tangu kuanzishwa Ijumaa wiki iliyopita, baada ya kumchapa vibao mshiriki wa Afrika Kusini, Luclay.
Akizungumza na waandishi wa habari kwa nyakati tofauti, mshiriki huyo alisema kutolewa kwake kulikuwa sawa kutokana na kanuni za shindano hilo kutoruhusu kushambuliana kwa matusi ama kupigana.
“Nilipoambiwa kuwa nimetolewa niliridhika, ingawa sikuwa katika hali nzuri, lakini hakukuwa na namna nyingine zaidi kutoka kwa kuwa nilifanya kosa,” alisema Lotus.
Chanzo cha mshiriki huyo wa Tanzania kumpiga kibao Luclay kilianzia wakati walipopewa kazi ya kufanya na Biggie ya kujaza majina ya fedha mbalimbali duniani.
Katika kazi hiyo Lotus aliweza kujaza nchini mbalimbali na kushindwa kumalizia nchi kama India, Afrika Kusini hata Tanzania, jambo lililoonekana kumkera Luclay na kumuuliza Lotus kisa cha kuacha kujaza nchi hiyo ya Afrika Kusini.
Lotus alieleza kuwa kushindwa kujaza nchi hizo si kwa kuwa hakufahamu majina ya fedha hizo, bali ni kutoka na karatasi walizopewa zilikuwa na kurasa nne, hivyo yeye alijaza bila kufuata mtiririko na muda ukamalizika na yeye kushindwa kumalizia.
“Karatasi za nchi tulizopewa kujaza majina ya fedha zilikuwa na kurasa nne na mimi sikujaza kwa kufuata mtiririko, hivyo muda ulikwisha bila ya mimi kujaza nchi hizo, ikiwemo nchi yangu ya Tanzania, pamoja na sula la muda pia nchi zilikuwa katika kurasa za mwisho,” alisema Lotus.
Lotus alisema kuwa pamoja na kumueleza yote hayo Luclay, alionekana kuendelea na mzozo huo kuwa ni kwa nini aliacha Afrika Kusini na huku ndiko katika ardhi yake.
“Luclay aliendelea kusumbua juu ya sula hilo nami nilimtaka kuachana nalo na kunyamaza, lakini hakufanya hivyo, ndio chanzo cha mimi ‘kumslap’.”
Pia Lotus alipotakiwa kujibu ni kwa nini alimtaja mshiriki mwenzake kutoka Tanzania, Bhoke, katika orodha ya watu waliotakiwa kutoka wiki iliyopita, alisema ni sehemu ya mchezo na wala hakuwa na maana nyingine.
“Sina uadui na Bhoke, pia kutoka nchi moja si kama ni marafiki, lakini ule ni mchezo, unapokuwa kwenye mchezo unaowaona ni wachezaji na si bendera ya nchi, kwa hiyo ilikuwa sehemu ya mchezo hivyo watu wasinifikirie vibaya.”
Akieleza kutoka mapema kwa kosa hilo, alisema kuwa hata kama asingefanya kosa hilo angeweza kutolewa mapema pia, lakini jambo kubwa anashukuru amepata marafiki.
“Kuingia BBA si kufuata ‘bingo’, bali ni kwa ajili ya kujifunza mambo mengi na kupata marafiki, hakuna njia ya kupata marafiki wengi kwa urahisi kama namna hii.
“Nimepata marafiki, kwa sasa naweza kwenda kokote na nikakutana na marafiki zangu, BBA si fedha tu, ni pamoja na kujifunza na kupata ‘network’.”
Lotus aliweka wazi kuwa hana uadui na Luclay na atakapokutana naye atambusu na kukumbatiana naye vizuri tena kwa furaha.
“Watu wanafikiria vibaya lakini mimi si mtu wa hasira, nikikutana na Luclay nitamchangamkia tena vizuri, nitakumbatiana naye kwa furaha na nitampiga ‘kiss’.”
Lotus ambaye ni mtangazaji wa kituo cha televisheni cha EATV katika kipindi cha Nivanna, pamoja na kueleza yote lakini hakuweka wazi juu ya mipango yake ya kurudi kazini.

Washiriki wa BBA waliyopigiwa kura za kubaki katika shindano hilo na alama zao walizopata na asilimia.
Vina 41.51 % (2929)
Confidence 30.26 % (2135)
Sharon 15.56 % (1098)
Bernadina 7.54 % (532)
Michael 5.13 % (362)
Total votes: 7056

Washiriki wa BBA wanaopendwa na mashabiki wengi na alama pamoja na kura walizopata washiriki hao.
Vina 12.51 % (346)
Confidence 11.71 % (324)
Luclay 9.26 % (256)
Sharon 9.15 % (253)
Karen 7.70 % (213)
Hanni 6.15 % (170)
Wendall 5.89 % (163)
Alex 5.50 % (152)
Weza 5.06 % (140)
Lomwe 4.48 % (124)
Zeus 3.15 % (87)
Ernest 2.89 % (80)
Nic 2.89 % (80)
Bhoke 1.99 % (55)
Vimbai 1.45 % (40)
Felicia 1.41 % (39)
Millicent 1.37 % (38)
Lotus 1.16 % (32)
Nkuli 1.16 % (32)
Jossy 1.01 % (28)
Mumba 0.94 % (26)
Miss P 0.90 % (25)
Kim 0.80 % (22)
Micheal 0.58 % (16)
Bernadina 0.54 % (15)
Danny 0.36 % (10)
Jumla ya kura: 2766

Mwandishi wa habari wa Gazeti la The African, Sidi Mgumia akifanya mahojiano na Lotus
Lotus akizungumza



Akinena

No comments:

Post a Comment