Tuesday, July 5, 2011

HAWA NDIYO WAREMBO WALIOPITISHWA KUINGIA KAMBI YA REDDS MISS ILALA 2011







Meneja Masoko wa Kampuni ya bia Tanzania TBL Fimbo Butallah akisalimiana na warembo wanaoshiriki katika shindano la Redds Miss Ilala 2011 wakati wa uzinduzi wa kambi ya warembo hao leo (Picha kwa hisani ya Mtaa kwa mtaa Blog).

Warembo wafuatao kutoka katika katika vituo viwili vya Dar City Centre na Tabata wamefanikiwa kupitishwa na Kamati ya Miss Ilala kuingia kwenye kambi ya Miss Ilala inayo anza tarehe 4 Julai 2011. Warembo watakutana katika hotel ya Lamada Jumatatu saa nne kwa kwa ajili ya semina na kukamilisha taratibu zote za usaili ikiwa ni pamoja na kuingia mikataba na Dar Metropolitan promotions.






  1. Jenifer Kakolaki 12. Alexia William

  2. Meryvine Kenzia 13. Patricia Kajubi

  3. Salha Israel 14. Lilian Paul

  4. Diana John 15. Judith Mlingwa

  5. Nasra Salim 16. Cresencia Haule

  6. Godliver Mwashamba 17. Williet Wilson

  7. Faizal Ally 18. Priscilla Mchemwa

  8. Augostina Mshanga 19. Ritha Cuthbert

  9. Lilian Bryceson 20. Maria John

  10. Lilian William 21. Edna Mnada

  11. Mariam Manyanya


Shindano la Redds Miss Ilala 2011 linategemewa kufanyika siku ya Vunja jungu katika ukumbi ulioko katikati ya jiji la Dar es salam.





Mpaka sasa hivi wadhamini waliojitokeza kudhamini Shindano hilo ni Redds Original inayozalishwa na kiwanda cha Tanzania Breweries Limited ambao ndio wadhamini wakuu, wengine ni Vodacom Tanzania, Tanzania Standard Newspapers, Fabak Fashion, TV Sibuka, Maisha Club, na 88.4 Clouds FM na Paris Pub ya Tabata.





Watakapokuwa kambini warembo watajifunza mambo mbali mbali yanayohusu mashindano ya urembo, mambo ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kibiashara. Pia watajifunza namna ya kujitunza kama wasichana na kufanya shughuli za kijamii. Warembo pia wanategemewa kufanya michezo mbali mbali, kuonyesha vipaji na kufanya ziara ya kitalii.


No comments:

Post a Comment