Saturday, August 6, 2011

AIRTEL yamwaga msaada wa vyerehani 10 kwa watoto yatima Dar es Salaam


Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Tunu Kavishe (kulia) akikabidhi moja ya mashine za kushonea cherahani kwa Mwakilishi wa Kikundi cha Wanawake cha Kulelea Watoto Yatima cha Msasani , Yonnes Kihiyo katika hafla iliyofanyika jijini Dar es Salaam leo.

Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Tunu Kavishe (kushoto) akikabidhi moja ya mashine za kushonea cherahani kwa Mwakilishi wa Kikundi cha Wanawake cha Kulelea Watoto Yatima cha Kawe Huruma Group, Hilda Rwebangira katika hafla iliyofanyika Jijini Dar es Salaam.
Kampuni ya simu za mikononi ya AIRTEL imetoa msaada wa vyerehani 10 kwa vikundi vitatu vya wanawake vinavyolea watoto yatima jijini Dar es Salaam ili kuviongezea uwezo wa kulea watoto wanaolelewa katika vituo hivyo.

Msaada huo umekabidhiwa na Meneja Huduma za Jamii wa Airtel, Tunu Kavishe kwa vikundi hivyo, ambavyo ni kikundi cha Wanawake cha Kulea Watoto Yatima cha Msasani, Kikundi cha Huruma cha Kawe pamoja na kile cha kulea watoto yatima cha Kinondoni.

Akizungumza wakati wa makabidhiano hayo yaliyofanyika jijini leo, Bi. Kavishe alisema Airtel itaendelea kugawa misaada kwa vikundi vya wasiojiweza ikiwa ni sehemu ya kampeni yake ya kusaidia jamii katika kutatua baadhi ya matatizo ambayo inayakabili hususani katika sekta ya elimu.

Akipokea msaada huo wa mashine za kushonea, Mwakilishi wa Kikundi cha Wanawake cha Kulelea Watoto Yatima cha Msasani (Womens and Orphans Centre), Prudencia Kibatara alisema msaada huo utawasaidia katika kuboresha utoaji wa huduma kwa watoto hao ambao twanawahudumia katika kituo hicho.

" Tunachangamoto nyingi ikiwemo idadi kubwa ya watoto na kipato kidogo cha uendeshaji vikundi hivi, hivyo tunawapongeza sana Airtel kwa kushirikiana nasi katika kusaidia jamii. Kupitia cherehani hizi tutaanzisha madarasa ya ushonaji na ada zitakazolipwa zitatumika kusaidia watoto hawa, vilevile chereharani hizi zitatumika kushona vitambaa na mashuka ambayo yataleta pato katika vikundi na tutaweza hata kuendelea kuwasomesha watoto hawa vizuri" alisema, Bi Kibatara.

Aidha Afisa Mtendaji wa Kata ya Msasani , Bw. Swai aliipongeza kampuni ya simu ya Airtel kwa kujitokeza na kusaidia vikundi hivyo na kutoa angalizo kwa walezi wa vikundi hivyo kutumia msaada huo kwa manufaa ya watoto na si yao binafsi.

"Jamani wakina mama naomba huruma zetu za dhati ziendelee hakikisheni mnaendelea kutumia msaada huu mlioupata kama nyenzo ya kuendelea kuwatunza na kusaidia watoto hawa na sio kujifaidisha sisi wenyewe" alisema Bw. Swai.

.."Leo Airtel wameonyesha jinsi wanavyojali jamii wanayoihudumia hivyo naomba tuwaunge mkono ili dhamira yao itimie" alisisitiza Bw. Swai.

Vituo vilivyopata msaada huo viko jijini Dar es salaam ambavyo kwa ujumla vyote vinalea watoto wasiopungua 40 kila kimoja. Watoto wanaolelewa katika vituo hivyo bado wanamahitaji mengi japo kampuni ya simu za mkononi airtel imeweza kujitolea msaada huo wa vyerehani bado pia wanahitaji vifaa vya shule, vifaa vya kujifunzia, chakula pamoja na malazi ya kila siku.

Airtel imekuwa mstari katika kusaidia uboreshaji wa maisha ya jamii kwa kutoa misaada ya aina mbalimbali na kudhamini shughuli za miradi ya maendeleo.bado Airtel inampango wa kutoa msaada wa cherehani pia katika mikoa ya mwezi huu kwa dhumuni la kuendelea kupunguza tatizo la kipato kwa vituo vya wananchi wanaoishi katika mazingira magumu.

No comments:

Post a Comment