Wednesday, August 10, 2011

Kutoka Viwanja Vya Bunge Mjini Dodoma









Waziri wa Nishati na Madini, William Ngeleja, akitoa Tamko rasmi kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuhusu upatikanaji wa mafuta nchini ndani ya ukumbi wa vikao vya Bunge.


Mbunge wa Ubungo (CHADEMA) John Mnyika, akichangia kuhusu tatizo la upatikanaji wa mafuta nchini.


Mbunge wa Korogwe mjini (CCM) Yusuph Abdallah Nassir, akichangia hoja binafsi ya dharura aliyoiwakilisha Mbunge wa Bumbulu January Makamba kuhusu tatizo la mafuta nchini, ambalo jana jioni Waziri wa Nishati na Madini William Ngeleja ameasilisha Tamko la Serikali kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Mbuge wa Kinondoni, Idd Azan akichangia kuhusu janga la mafuta.


Mbunge wa Rombo (Chadema) Joseph Selaini akichangia


Naibu Waziri wa Viwanda na Biashara ,Nyalandu akiteta jambo na Makamu wa Pili wa Rais, wa Zanzibar, Bungeni Dodoma


Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma ya Bunge ya Hesbu za Mashirika ya Umma, Kabwe Zuberi Zitto, akizungumza na waandishi wa habari mjini Dodoma jana, kuhusu Kamati yake iliyomuandikia barua Spika wa Bunge ikimuomba aridhie mapendekezo ya wabunge wataounda kamati ya Bunge chini ya Kamati hii ya Kudumu ya Bunge ya hesabu za Serikali na Mashirika ya Umma, ili ichunguze sakata zima la uuzwaji wa shirika la UDA


abunge wakibadilishana mawazo nje ya viwanja vya Bunge Dododma leo (kulia) Ritta Kabati (viti maalumu), (kushoto) Rajab Mbarouk Mohammed (CUF-OLE) na Prof. Kulikoyela Kahigi (CHADEMA-Bukombe) mwenye miwani.


Baadhi ya waandishi wa habari wakimsikiliza Mwenyekiti wa Kamati ya Huduma ya Bunge ya Hesabu za Mashirika ya Umma Kabwe Zuberi Zitto.Picha Zote na Mwanakombo Juma-MAELEZO

No comments:

Post a Comment