Thursday, August 4, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ATEMBELEA MAONYESHO YA NANE NANE DODOMA

Makamu wa Rais wa Jamhuri wa Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijaribisha kuwasha Trekta la kilimo, baada ya kumkabidhi funguo ya Trekta hilo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais Mazingira, Teresia Huvisa (kushoto) kwa ajili ya matumizi ya kilimo, wakati wa hafla ya maadhimisho ya mwaka wa pili wa utekelezaji wa Kaulimbiu ya Kilimo Kwanza leo, ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya Nane Nane zinazoendelea katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.

Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Ghrarib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mfugaji wa Kuku, Halimi Amiri, alipotembelea katika banda la Wilaya ya Chamwino katika maadhimisho ya sikukuu ya Wakulima Nane Nane, leo Agost 03, 2011, wakati wa hafla ya maadhimisho ya mwaka wa pili wa utekelezaji wa Kaulimbiu ya Kilimo Kwanza leo.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Mkurugenzi wa Mazingira Ofisi ya Makamu wa Rais, Julius Niingu, wakati alipotembelea katika Banda la Ofisi ya Makamu wa rais. Wa pili kulia ni Mama Asha Bilal, wa pili (kushoto) ni Mkurugenzi wa Utawala na Rasilimali watu, Ofisi ya Makamu wa Rais, Deo Magazeni.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia moja ya Tela la Trekta linalotengenezwa nchini, wakatiti wa wakati wa hafla ya maadhimisho ya mwaka wa pili wa utekelezaji wa Kaulimbiu ya Kilimo Kwanza leo, ikiwa ni sehemu ya maonyesho ya Nane Nane zinazoendelea katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa mwalimu wa Shule ya Msingi Bwigiri Wasioona, Achimpota Nicolaus na kumtazama mmoja wa wanafunzi wasioona, Hasanat Athuman, kuhusu jinsi wanavyowafundisha wanafunzi wasioona, wakati alipotembelea katika Banda la Wilaya ya Chamwino kwenye maonyesho maadhimisho ya sikukuu ya Nane Nane yanayoendelea katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.
Makamu wa rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa Kilimo na Mbogamboga na Matuda, Hery Ndumukwa, kuhusu zao la Nyanya.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akijaribu kubeba shina la Muhogo, wakati alipokuwa akitembelea mabanda ya maonyesho katika viwanja vya Nzuguni Nane Nane mjini Dodoma leo Agosti 03.
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiangalia na kusikiliza maelezo kutoka kwa Ofisa kutoka Kituo cha kudhibiti Panya Mkoa wa Morogoro, Eugen Ngolohela, kuhusu Panya aina ya Ndezi na wengineo, wakati alipotembelea katika mabanda ya maonyesho ya Maadhimisho ya Nane Nane leo, katika Viwanja vya Nzuguni mjini Dodoma.

No comments:

Post a Comment