Friday, August 5, 2011

NAPE ATEMBELEA CHANAL TEN

NA BASHIR NKOROMO

HATUA ya kuwataka watuhumiwa wa ufisadi wapime na kuchukua uamuzi wa kuondoka katika vikao vya maamuzi ya CCM kutakifanya Chama kuaminiwa zaidi na wananchi kuliko kikiwaacha.

Hayo yalisemwa jana mjini Dar es Salaam na Katibu wa Halmashauri Kuu ya CCM, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akizungumza na viongozi wa Kampuni ya Africa Media Group inayomiliki vyombo kadhaa vya habari kikiwemo kituo cha Televisheni cha Chanel Ten.

Alisema, hadi CCM inafikia hatua ya kupitisha maamuzi kadhaa ikiwemo kuwataka watuhumiwa wa ufisadi kuima na kuchukua hatua za kujitoa kwenye ngazi za maamuzi ndani ya Chama, Chama kilikuwa hakina namna nyingine ila kufanya hivyo kama kinapenda kuendelea kuongoza nchi.

"Hali ambayo chama kilikuwa kimefikia, ilikuwa kama kinataka kuendelea kuaminiwa na wananchi na kuongoza nchi, lazima kuchukua hatua hizo au kuacha uchukua hatua hizo kisiaminiwe kife", alisema Nape.

Alisema, kutokana na misingi ya CCM iliyowekwa na Waasisi wake chini ya hayati Mwalimu Nyerere, Chama kiliona kuwa bado kina wajibu wa kuongoza nchi na ili kiweze kujihalalishia kuongoza lazima kifanye mabadiliko.

Nape alisema, kimsingi mabadiliko hayo ambayo yalipitisha maamuzi zaidi ya 20, ni miongoni mwa mengi ambayo CCM imekuwa ikiyafanya tangu wakati wa TANU, na hivyo watu wasichukue muda mwingi kuyashangaa lakini washiriki zaidi katika utekelezaji.

Alisema maamuzi yaliyopitishwa na CCM lazima yataathiri baadhi ya watu, na kufafanua kwamba hilo halitakuwa jambo la ajabu kwa sababu mabadiliko yoyote yanapotokea huwa lazima yaathiri watu kwa namna moja au nyinvgine.

"Siwezi kusema hakuna watakaoathiriwa na mabadiliko haya, wale waliokuwa wananufaika na mfumo holela uliokuwa unawapa mwanya kufanya mambo kwa manufaa yao hata kama yanaathiri taifa, lazima wataguna na kujaribu kufanya sarakasi za kupinga mabadiliko haya", alisema Nape.

Alisema, ni kutokana na sababu hizo, ndio maana sasa zimetokea changamoto za hapa na pale katika mapokeo ya mabadiliko yaliyofanywa na CCM, ikiwemo baadhi kujaribu kujitokeza na kusema hadharani kwamba mabadiliko haya hayana maana.

Nape aliataka Watanzania hasa vyombo vya habari kuacha kusikiliza yanayosemwa mitaani nje ya vikao kwa sababu, badala yake, washike yaliyotamkwa na kupitishwa katika vikao vya CCM, nakuongeza kwamba milango bado ipo wazi vikaoni kwa kila mwenye hoja mbadala na maamuzi ya sasa.

Katika ziara hiyo viongozi wa Africa Media Group akiwepo Mkurugenzi Mtendaji, wake Hamza Kasongo walipata fursa ya kumsikiliza Nape na baadaye kumuuliza maswaliyasiyo na mipaka. Ziara hiyo ni mwendelezo wa ziara zake za kufahamiana na vyombo vya habari ambazo alianza kufanya tangu mwezi uliopita.

No comments:

Post a Comment