Monday, August 8, 2011

TAASISI YA THE FADHAGET DEVELOPMENT HOPE YATOA VIFAA VYA MICHEZO KWA ACOT SPORTS CLUB YA MTONI




Tunapenda kumshukuru Dr. FADHILI EMILY ambaye ni mkurugezi wa taasisi ya THE FADHAGET DEVELOPMENT HOPE wanahousika na kusaidia jamii, kutunza mazingira, kupiga vita madawa ya kulevya, migogoro ya mke na mume, umasikini na njaa. Tayari wamekwisha fungua kituo cha afya Tandika wana mitambo maalumu ya vipimo vya magonjwa ya aina zote na wana tengeneza dawa kwa kutumia matunda na mimea asilia. Kwa kuweza kutusaidia jezi seti moja na mipira miwili .

Ndugu wahariri,wanahabari na watanzania kwa ujumla ni furaha kwetu kuwaona mmefika hapa , siku hii ya leo,kwa kweli mnaitaji pongezi za pekee siku hii ya leo.

HISTORIA YA TAASISI

ACOT ni taasisi isiyo ya kiserikali ilianza rasmi 30/10/2010. Ni taasisi ambayo inatambuliwa na Serikali kwa kuwa tumepata usajili rasmi toka Serikalini. makazi yake ni mtoni kwa Aziz Ally, wilaya ya Temeke mkoa wa Dar es salaam. Sababu zilizotufanya tuanzishe ni nyingi lakini moja ya sababu hizo ni Kukuza na Kuendeleza vipaji vya vijana, Kielimu,Kiutamaduni na Kimichezo.

Baada ya kuona vijana wengi hasa wa wilaya yetu ya Temeke wanaishi katika mazingira magumu na pia wana vipaji tofauti ila wamekosa mtu wa kuwasimamia na kuwaendeleza pamoja na kuwapatia mahitaji muhimu kama vile chakula,maradhi na vifaa.

sisi tukiwa kama watanzania tumeona tujitokeze mbele yenu ili mtusaidie pale ambapo tumefikia ili tuweze kuwaendeleza baadhi ya vijana kimaisha maana vijana ni nguvu kazi ya Taifa. Tunajua kuwa kwamba tunadeni kubwa kwetu na Taifa letu la Tanzania hivyo kuendelea kuwaacha vijana hawa ni kupoteza muelekeo wetu.

CHANGA MOTO TUNAZO PATA

Kunachanga moto nyingi tunazo pata katika maisha haya ya kuwalea vijana lakini moja ya changamoto hizo ni ukosefu wa vifaa vya michezo na utamaduni kama vile Viatu,Mipira, Jezi,Bipsi,Koni,Nyavu, Shine Guard,Ngoma.

Pia Ukosefu wa Ada kwa ajili ya kuwaendeleza wachezaji wetu na wanajamii wetu kielimu zaidi.

Upungufu wa dawa za kuchukua,Clip bandage,diclopa,diclofenac,glucose,deepheat spray,na Chakula kama vile mchele,sukari,sembe.

Fedha za kuendeshea programu mbalimbali kwa maendeleo ya jamii yetu husika.

MAFANIKIO

Mafanikio tuliyoyapata tangu kujumuika kwetu ni pamoja na kusikilizana sisi kwa sisi kuwaelimisha vijana wenzetu kuhusu Ukimwi,Matumizi ya Kondom,Ujasiriamali kuachana na madawa ya kulevya kwa wale wanaotumia,Kuanzisha vikundi kulingana na fani zao ili kukuza vipaji vyao.

Kupitia vijana wetu tumeweza kuanzisha timu ya mpira wa miguu na imeweza kushiriki mashindano ya EAST AFRICA CUP 2011.Timu zilizoshiriki U16 ni kumi na nne Kutoka Kenya,Uganda,Zimbabwe,Zanzibar na Tanzania na tukafanikiwa kuwa washindi wa pili U16 na kuiletea sifa mtaa wetu,wilaya yetu hata mkoa wetu.

Kupitia mashindano hayo tumeweza kupata marafiki wengi wa kigeni kutoka nchi sita wanawataka wachezaji wetu wakacheze kwao.

Kupitia vijana wetu tumeweza kuanzisha kikundi cha ngoma za asili,na kuwafundisha ngoma mbalimbali za makabila tofauti kama vile Masewe,Mangaka,mganda wa kikutu,lingokwa,lumbunjumu na likaturinge,kupitia sanaa yao hiyo wameweza kupata marafiki wakigeni kutoka nchini Kenya na kikundi cha sanaa cha haba na haba kilichopo nchini Kenya .

Tunawasomesha vijana wetu katika shule za Msingi (vijana 6) ,Sekondali (vijana 20), vyuo vya ufundi stadi (vijana 5) na hata vyuo vikuu (vijana 3) na shule ya walemavu (2) wasichana na wavulana.

Pia tumeweza kuwapeleka vijana sita katika mafunzo ya UJASIRIAMALI katika chuo kikuu cha DSM Mlimani kitengo cha ujasiriamali (UDEC) yaliyofanyika 25/07/2011 mpaka 29 /07/2011 na kupata vyeti.

HITIMISHO

Pamoja na maelekezo yote haya ni vyema mkajua kuwa sisi mpaka sasa tupo katika wakati mgumu endapo kunatokea mashindano au mwaliko wowote ule,tatizo ni vitendea kazi hatuna na akuna sehemu, tunayojua kuwa tutaenda kusaidiwa.

Tunaomba sana tusaidiwe vitendea kazi kama vile,Kompyuta,Projector,Digital camera,Viatu vya Mpira(Njumu),Mipira, Jezi,Bipsi,Koni,Shine Guard itakuwa vizuri sana, kwani tunataka tuwe mfano wa kuigwa katika wilaya yetu ya Temeke na kata yetu ya mtoni na mtaa wetu wa sabasaba na hata taifa kwa ujumla.

Asanteni sana kwa kuweza kunisikiliza kama kuna mapungufu mtatusamehe lakini ni imani yetu tuta kuwa tumeeleweka mungu wabariki wote waliofika hapa siku hii ya leo.

Mungu ibariki Afrika, Mungu ibariki Tanzania, Mungu ibariki ACOT

Wenu Katika Ujenzi wa Taifa

Emmanuel Mwampishi.

Mkurugenzi

No comments:

Post a Comment