Tuesday, August 30, 2011

TTCL YAENDELEA KUTOA MSAADA ZAIDI KWA WAHITAJI







TTCL jana ilitoa msaada wa vyakula kwa watoto walemavu wa shule ya Msingi Uhuru mchanganyiko pamoja na watoto wasiojiweza wa kituo cha SOS kilichopo kandokando ya barabara ya Sam Nujoma, Mwenge.





Msaada huu wa chakula unalenga kusherehekea sikukuu ya Idd El-Fitr pamoja na watoto hawa ambao kwa namna moja au nyingine ni kundi linalohitaji kusaidiwa na jamii inayolizunguka.




TTCL kama kampuni ya umma na ya kizalendo inajali sana jamii



inayoizunguka pamoja na matatizo yake ndio maanaimeamua kutoa msaada huo wa vyakula kwa makundi haya ya watoto wahitaji ni wazi kuwa ni jukumu letu kama TTCL, kampuni ya kitanzania kusaidia jamii.



Msaada huu kwa vikundi hivi viwili una thamani ya shilingi milio


ni Mbili (2 m/=). Niseme tu kuwa ni utamaduni wetu sisi TTCL kuwa wakarimu si tu kwa kundi hili bali hata kwa makundi mengine yenye mahitaji katika jamii ye


tu ya kitanzania.





Kuthibitisha hilo, Afisa Mtendaji Mkuu



wa TTCL ametoa msaada wa vyakula kwa ajili ya sikukuu ya Idd Elfitr kule Moshi Kilimanjaro kwa vikundi vya wazee, yatima na walemavu wa viungo vya mwili.





Jumla ya vikundi vitatu vitafaidika na msaada wa vyakula wenye thamani ya shilingi milioni moja na laki tano (1.5millioni).





TTCL Inaahidi kuendelea kuhudumia jamii yetu pale kampuni inapofanya vizuri na mapato kuongezeka kwani ndio njia mojawapo ya kurudisha baadhi ya mapato kwa wateja wetu.




Tunashukuru kwa ushirikiano mzuri kati ya TTCL na watanzania Tunaomba tusaidiane kupinga hujuma zozote dhidi ya mtandao na kampuni ya TTCL kwa ujumla.

No comments:

Post a Comment