Wednesday, August 17, 2011
YOHANA ROBART APANIA KUMDUNDA MKENYA IDDI PILI MOROGORO
BONDIA Yohana Robert ameapa kumsambaratisha mpinzani wake kutoka Kenya James Unyango katika raundi za kwanza la pambano lao.
Pambano hilo linatarajia kuwa katika uzito wa kg 61 katika raundi 6 ambapo litafanyika Sikukuu ya IDD pili katika uwanja wa Jamuhuri, Morogoro.
Pambano hilo litakuwa ni moja kati ya mapambano ya utangulizi katika pambano la marudiano kati ya Francis Cheka na Mada Maugo.
Akizungumza Dar es Salaam jana, Yohana alisema, katika mapambano hayo pambano lake ndio linahusisha bondia kutoka nje ya nchi hivyo atajitahidi kuhakikisha ushindi huo unabaki hapa nchini.
"Siwezi kuwaangusha Watanzania na wapenzi wa ngumi kwa ujumla ntahakikisha na msambaratisha mpinzani wangu mapema katika raundi za awali na kuuacha ushindi hapa nyumbani," alisema Yohana.
Alisema, kwa sasa yupo kambini Gongo la mboto chini ya kocha wake Habibu Kinyogoli ambapo anajifua ili kuweza kukabiliana na mpinzani wake huyo.
Cheka na Maugo wanarudiana baada ya kushindana kwa pointi moja katika pambano lao la kufunga na kufungua mwaka lililofanyika katika ukumbi wa PTA ambapo Cheka alimzidi Maugo kwa pointi ambapo Maugo alipinga matokeo hayo.
Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na huzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones na wengine kibao.
DVD hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha maarufu Rajabu Mhamila 'SUPER D BOXING COACH' hapo
na kwa Dar es Salaam DVD hizo zinapatikana katika Makutano ya Barabara ya Uhuru na Msimbazi
No comments:
Post a Comment
‹
›
Home
View web version
No comments:
Post a Comment