Thursday, September 15, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL MGENI RASMI KUMBUKUMBU YA MIAKA 35 YA RELI YA TAZARA


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya Tazara kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Maonyesho hayo yamefanyika leo Septemba 14 katika Viwanja vya Tazara jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Tazara, Mkandarasi Abdallah Shekimweri, wakati akitembelea mabanda ya maonyesho kwenye maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya Tazara na maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania katika viwanja vya TAZARA jijini Dar es Salaam leo Septemba 14. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akitoka katika moja ya mfano wa Behewa la Daraja la kwanza la Treni ya TAZARA, wakati alipokuwa katika maonyesho ya TAZARA, wakati wa maadhimisho ya miaka 35 ya shirika hilo sambamba na maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania, iliyofanyika katika viwanja vya TAZARA jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Meneja wa Tazara, Mkandarasi Abdallah Shekimweri, kuhusu matumizi ya Kibelenge wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho kwenye maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya TAZARA kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Maonyesho hayo yalifanyika leo Septemba 14 katika Viwanja vya Tazara jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kuhusu mataluma ya Reli na matumizi yake wakati alipokuwa akitembelea katika mabanda ya maonyesho kwenye maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya TAZARA, kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Maonyesho hayo yamefanyika leo Septemba 14 katika Viwanja vya Tazara jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi aliyekuwa Waziri wa Wizara ya Uchukuzi miaka ya nyuma, Job Lusimbe, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake katika ujenzi na maendeleo ya Reli ya TAZARA, wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya Tazara kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Maonyesho hayo yamefanyika leo Septemba 14 katika Viwanja vya Tazara jijini Dar es Salaam. Picha na Muhidin Sufiani-OMR
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akimkabidhi zawadi mzee John Nchimbi na mkewe, Sylviaa Nchimbi, waliokuwa ni abiria wa kwanza kusafiri na Reli ya TAZARA mwaka 1976, ikiwa ni sehemu ya kutambua mchango wake katika ujenzi na maendeleo ya Reli ya Tazara, wakati wa maadhimisho ya Kumbukumbu ya miaka 35 ya reli ya Tazara kuelekea maadhimisho ya miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania. Mzee Nchimbi na mkewe wamepewa zawadi ya kusafiri na treni ya TAZARA bure katika kipindi chote cha maisha yao. Picha na Muhidin Sufiani-OMR

No comments:

Post a Comment