Friday, September 9, 2011

SERIKALI YAOMBA UFUNDISHWAJI WA MAKOCHA MPIRA WA KIKAPU USA


SERIKALI kupitia kwa Naibu Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Fennella Mkangara imeuomba Ubalozi wa Marekani nchini kuwapeleka wachezaji wa Tanzania kujifunza Kikapu nchini mwao.

Akizungumza Dar es Salaam juzi, kabla ya kufunga kliniki ya watoto chini ya Umri wa miaka 16 iliyofadhiliwa na Ubalozi huo, Mkangara alisema Serikali ya Tanzania inawashukuru kwa msaada wao kuisaidia Tanzania kujifunza Kikapu kwa namna mbalimbali.

Alisema Serikali inautambua mchango wao na kuahidi kutoa uangalizi wa karibu kwa Shirikisho la Mchezo huo nchini, TBF kuwaendeleza watoto waliopata mafunzo ya awali kutoka kwao.

"Kwa niaba ya Serikali tunawashukuru sana ubalozi wa Marekani kwa mchango huu, nimeambiwa hii ni zaidi ya mara moja kutoa msaada katika kliniki kama hii, kwa niaba ya serikali nasema tena asanteni na tunaomba muendelee kutusaidia ikiwezekana mafunzo haya tukapate nchini Marekani na sisi tuwapate wachezani kama Michael Jordan.," alisema.

Katika hatua nyingine Naibu Waziri ameliwaambia viongozi wa TBF kuepuka kulala na kuelekeza nguvu katika kuviendelea vipaji vilivyoibuliwa na kuihakikisahia kuwa Serikali ipo tayari kutoa ushirikiano wakati wowote itakapohitajika.

Aidha aliwahimiza wanafunzi waliopata mafunzo hayo pamoja na walimu kuanza kuyafanyia kazi mara moja ili kujijengea mazingira ya kuupenda na kuufahamu zaidi mchezo huo.

Kozi hiyo ya siku tatu iliendeshwa na wachezahi wa zamani waliowahi kutamba katioka Ligi za NBA na WNBA za Marekani, Dee Brown, Tamika Raymond, na Becky Bonner na kushirikisha watoto zaidi ya 100 kutoka mikoa mbalimbali Tanzania bara na Zanzibar.

No comments:

Post a Comment