Monday, September 12, 2011

SIKU TATU ZA MAOMBOLEZO........ SUMATRA hawawajibiki ipasavyo kukagua usafiri...!



KUFUATIA msiba mkubwa uliotokana na ajali ya kuzama kwa meli ya Spice Islander katika bahari ya Hindi usiku wa kuamkia Jumamosi, Septemba 10, 2011

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, ameamuru maombolezo ya kitaifa kwa muda wa siku tatu kuanzia leo tarehe 11 Septemba, 2011 ambapo bendera nchini zitapepea nusu mlingoti.
Aidha, kufuatia msiba huo, Mheshimiwa Rais, ameahirisha ziara rasmi ya kiserikali ya siku tatu nchini Canada ambako alikuwa amealikwa na Gavana Mkuu wa nchi hiyo, Mheshimiwa David Johnston.
Katika ziara hiyo iliyokuwa ifanyike kuanzia tarehe 14 – 16 Septemba, 2011, Mheshimiwa Rais angekutana pia na Waziri Mkuu wa nchi hiyo Mheshimiwa Stephen Harper. Mheshimiwa Rais ameiomba Serikali ya Canada kupanga ziara hiyo kwa tarehe za baadaye.
Rais alitembelea majeruhi katika Hospitali ya Mnazi Mmoja, Zanzibar, kuwajulia hali, baada ya ajali hiyo. Akiwa katika ziara hiyo ya majonzi aliarifiwa kuwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano ilikuwa imechukua maamuzi kadhaa kukabiliana na hali ya ukoaji wa watu katika ajali hiyo.
Miongoni mwa hatua hizo ni pamoja na kuchangia kiasi cha sh. milioni 300 ili kusaidia zoezi hilo ikiwa ni pamoja na kusaidia kusafirisha na kuzika miili ya watu waliopoteza maisha katika ajali hiyo. SMZ imetoa sh milioni 100 kwa shughuli hiyo.
Serikali ya Muungano pia imeamua kukubali msaada wa wapigaji mbizi kutoka Afrika Kusini kwa ajili ya kusaidia kufanya tathmini ya jinsi meli ilivyozama na kuokoa maisha ya watu ambao watakuwa wamebanwa ndani ya meli hiyo.
Aidha leo, Septemba 11, 2011, Kamati ya Taifa ya Ulinzi na Usalama itafanya kikao chake mjini Zanzibar kuzungumzia hali ya ajali hiyo kwa maana ya kupata maelezo kamili kuhusu ajali hiyo, kupokea ripoti ya ajali, kufanya tathmini ya ripoti hiyo na kutoa maelekezo ya jinsi ya kukabiliana na hali ya sasa na hali ya baadaye ya usafiri wa maji nchini.
Hata hivyo kabla ya kikao hicho, tayari Rais Kikwete ameamua kufanyika kwa uchunguzi wa kina kubaini chanzo cha ajili hiyo.

Kwa habari zaidi na Picha
BOFYA HAPA

MAMIA ya wananchi wakiwemo viongozi wakuu walimiminika katika viwanja vya Maisara na Hospital ya Mnazi mmoja pamoja na bandari kuu ya zanzibar ili kwenda kuona na watambuwa watoto wao wazee wao ambao walikuwepo katika meli iliyopata ajali huko Nungwi ikielekea kisiwani Pemba hapo jana

Waliomiminika katika sehemu hizo kutoka sehemu mbali mbali za Unguja kunafuatia habari zilizoanza kutangazwa jana katika vyombo mbali mbali vya habari kwamba chombo cha Spice kimezama na ni kwamba kilikuwa kimechukuwa abiria kikielekea Pemba

Kwa mujibu wa habari zilizokuwa zikisimuliwa na baadhi ya wananchi waliofika hapo maisara wamesema kuwa suala kubwa lililochangia kutokea ajali hiyo ni kuwa vyombo vimechoka sana na wengine wamesema kuwa kujaa sana kwa chombo hicho hapo jana pia ni sababu ambazo zilichangia tukio hilo

Katika Viwaja vya Maisara umati wa watu ulikuwa umejaa kupita kiasi halikadhalika hata Hospital ya Mnazi mmoja umati ulikuwa umejaa vikle vile lengo kubwa la kuwepo hapo ni kuona na kuwatambua vijana wao ambao wameruhiwa na ambao wanapata matibabu

Halikadhalika umati mkubwa ulikuwa umejazana sana katika bandari mkuu ya Zanzibar ambapo maiti na majeruhi wa ajali hiyo walikuwa wakifikia hapo kutoka sehemu ya tokeo

Kufuatia ajali hii hii itakuwa mara ya tatu
katika pindi cha nyuma meli ya MV Fathi ilizama 29/5/2009 ambapo watu kadhaa wafariki dunia na baadhi ya mizigo ilpotea kutokana na ajali hiyo iliyotokea hapo nyuma, pia maafa makubwa ya MV Bukoba 21/5/1999

Kufuatia tokeo hilo wananchi wa zanzibar leo walikuwa wamejikusanya vikundi kila sehemu kuzungumzia tukio hili ambalo limetoke hapo jana likiwa limeacha majonzi makubwa kutokana na msiba huo uliotokea hapa zanzibar

No comments:

Post a Comment