Friday, September 9, 2011
VIJANA NANE WACHAGULIWA MCHEZO WA KIKAPU
WACHEZAJI nane walio na umri chini ya miaka 16 waliofanya vizuri katika Kliniki ya watoto ya umri huo wamechagulia kushiriki fainali za Afrika zitakazoanza kesho na kumalizika keshokutwa Nairobi nchini Kenya.
Watoto hao kati ni 100 kutoka mikoa 15 Tanzania bara na Zanzibar walioshiriki kliniki ya siku tatu ya mchezo huo iliyoandaliwa na Shirikisho la Michezo huo nchini (TBF) kwa kushirikiana na Ubalozi wa Marekani pamoja na FHI Tanzania na kumalizika juzi Jijini Dar es Salaam.
Wachezaji waling'ara na kuchaguliwa na kuchaguliwa
Alex Peter, Siuba Said, Alinan Andrew, Mrumbi Issa, Raymond Alen na Rashid Mwinyi kutoka Dar es Salaam, John Matyeni, na Johnson Sabato kutoka Mara.
Mchujo wa wachezaji hao ulifanywa na nyota wa zamani wa Kikapu wa Ligi ya NBA na WNMB za Marekani, Tamika Raymond, Dee Brown na Becky Bonner waliokuwa nchini kuenesha kiliniki hiyo iliyomalizika juzi Jijini Dar es Salaam.
Akizungumza mara baada ya kumalizika kwa mchujo huo nyota aliyetamba katika Ligi ya NBA, Dee Brown alisema watoto wote walionesha uwezo mkubwa lakini hao walikuwa wakiwaongoza wenzao.
"Kwa furaha kubwa nawatangaza wachezaji hawa kwenda Nairobi, wote walifanya vizuri katika kliniki yetu mpaka leo inamalizika ingewezekana kila mmoja kwenda Nairobi lakini nafasi ni chache hawa watawawakilisha wenzao., alisema Dee Brown.
Katibu Msaidizi wa Shirikisho la Mpira wa Kikapu Tanzania (TBF), Michael Maluwe alisema wanaondoka Dar es Salaam leo kwenda Nairobi watakapoungana na wenzao kutoka nchi mbalimbali za Afrika kucheza fainali za watoto chini ya umri huo.
Mikoa 15 kutoka Tanzania bara na Zanzibar ilishiriki katika kliniki hiyo ni ambayo ilifadhiliwa na Ubalozi wa Marekani nchini kwa kushirikiana na FHI Tanzania pamoja na TBF.
No comments:
Post a Comment