Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (wa pili kulia) akipokea mfano wa hundi ya shs milioni 10 kutoka kwa Mshauri wa Mambo ya Habari wa Benki ya NBC, Redemptus Masanja zilizotolewa na NBC kama sehemu ya mchango wake kununulia gari la kubebea wagonjwa wa Kituo cha Afya cha Mt. Benedict kilichoko Kitunda nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. NBC pia imefungua akaunti maalumu kupata fedha zitakazosaidia kufanikisha ununuzi huo. Kushoto ni Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Songea, Norbet Mtega na wa tatu kushoto ni Mama Mkuu wa Shirika la Masista Wabenedictini, Sr. Maria Shukrani Mkonde.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki (wa pili kushoto) akizungumza na Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Songea, Norbet Mtega (kushoto) wakati wakitembelea jengo jipya la Kituo cha Afya cha Mt. Benedict katika hafla ya uzinduzi rasmi wa kituo hicho ambako Benki ya NBC kupitia Mshauri wake wa Mambo ya Habari, Redemptus Masanja (kulia) ilikabidhi hundi ya shs milioni 10 zitakazotumika kununulia gari la kubebea wagonjwa wa Kituo hicho. Wa pili kulia ni Sr. Maria Agnesia wa kituo hicho. Hafla hiyo ilifanyika jijini Dar es Salaam jana.
Wacheza ngoma ya asili wakitoa burudani katika hafla ya uzinduzi wa Kituo cha Afya cha Mt. Benedict hafla ambayo Benki ya NBC ilikabidhi hundi ya shs milioni 10 kwa ajili ya ununuzi wa gari la wagonjwa wa kituo hicho. NBC pia imefungua akaunti maalumu ili kukusanya fedha zitakazotumika kukamilisha ununuzi huo.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Said Meck Sadiki akizungumza kabla ya kupo mfano wa hundi ya shs milioni 10 kutoka kwa Mshauri wa Mambo ya Habari wa Benki ya NBC, Redemptus Masanja (kulia kabisa nyuma) zilizotolewa na NBC kama sehemu ya mchango wake kununulia gari la kubebea wagonjwa wa Kituo cha Afya cha Mt. Benedict kilichoko Kitunda nje kidogo ya Jiji la Dar es Salaam jana. Kushoto ni Askofu wa Kanisa Katoliki Jimbo la Songea, Norbet Mtega na kulia ni Mama Mkuu wa Shirika la Masista Wabenedictini, Sr. Maria Shukrani Mkonde.
No comments:
Post a Comment