Thursday, November 10, 2011

MAKAMU WA RAIS DKT BILAL ASAINI TAMKO LA VIONGOZI WA DINI KUHUSU MABADILIKO YA TABIA NCHI NA FOMU YA MADAI ‘PETITION’


Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisaini tamko la Viongozi wa dini kuhusu mabadiliko ya Tabia Nchi, Fomu ya madai, wakati wa Tamasha la Vijana la ‘Tunaimani kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi’ lililofanyika kwenye Viwanja vya Don Bosco Upanga jijini Dar es Salaam leo, ikiwa ni sehemu ya maandalizi ya vijana hao kuelekea Durban kushiriki katika Mkutano wa 17 wa Mabadiliko ya Tabia nchi unaotarajiwa kufanyika mwishoni mwa mwezi huu, nchini Afrika ya Kusini. Kushoto ni Askofu Mkuu wa Jimbo la Tabora na Mwenyekiti wa Viongozi wa Dini Nchini, Askofu Paul Ruzoka.
Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisoma hotuba yake wakati wa Tamasha la wakati wa Tamasha la Vijana la ‘Tunaimani kuhusu Mabadiliko ya Tabia Nchi’ lililofanyika kwenye Viwanja vya Don Bosco Upanga jijini Dar es Salaam leo
Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Fatuma Mussa, mwakilishi wa Tanzania ambaye ni miongoni mwa vijana watakaoelekea Durban katika mkutano wa 17 wa Mabadiliko ya Tabia nchi unaotarajia kufanyika mwishoni mwa mwezi huu nchini Afrika ya Kusini.
Baadhi ya wanafunzi wa shule za Msingi na Sekondari na Vijana mbalimbali waliohudhuria Tamasha hilo, wakicheza kwa pamoja moja ya burudani zilizokuwa zikitolewa katika viwanja hivyo.
Vija washiriki wa mkutano huo kutoka Mataifa mbalimbali wakiimba kwa pamoja wimbo maalum kuhusu mabadiko ya Tabia nchi mbele ya mgeni rasmi.

Lily Yekoye kutoka Ethiopia, mmoja wa vijana wanaokwenda kushiriki katika mkutano huo, akielezea ujumbe wake mbele ya mgeni rasmi kuhusu mabadiliko ya Tabia Nchi katika nchi yake.

Nisengwe Regis, kutoka Rwanda akitoa ujumbe wake kuhusu mabadiliko ya Tabia nchi katika nchi yake.

Vijana wanaokwenda kushiriki katika mkutano huo Durban Afrika ya Kusini, wakiwa katika picha ya pamoja wakati wakijidaa kwa pozi la picha na Mgeni Rasmi Makamu wa Rais Dkt Bilal.

Wasanii Vijana kutoka nchini Botswana, wakishambulia jukwaa kwa burudani.
Picha ya pamoja.

No comments:

Post a Comment