Sunday, November 20, 2011

SAFARI YA TIMU YA TAIFA KWENDA MALAWI YAOTA MBAWA YAGEUKA ZIARA YA MIKOA TANZANIA BAADA YA KUCHAPWA NA TIMU YA MBEYA


Wachezaji wa timu ya Taifa ya Pool, ilipokuwa ikiwasili Mkoani Iringa wakati ikiwa safarini kuelekea Malawi, ambapo safari hiyo imeota mbawa na kuwa ni ziara ya mikiani.
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager imetangaza rasmi kufutwa kwa mashindano ya 'ALL AFRICA CUP 2011-BLANTYRE- MALAWI' yaliyotarajiwa kuanza Novemba 22, hadi 26, 2011.

Akitangaza mabadiliko ya safari hiyo, Meneja wa bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo, alisema kuwa Pamoja na mashindano hayo kufutwa Bia ya Safari, imeandaa ziara ya timu ya Taifa ya Pool katika mikoa ifuatayo ya Dodoma, Manyara, Arusha, Kilimanjaro na Tanga baada ya kushauriana na chama cha mchezo huo ili kuwafanya wachezaji wa timu ya taifa kuwa katika hali ya mchezo na kufanya mazoezi baada ya kuahirishwa kwa mashindano hayo yaliyokuwa yafanyike Malawi.

Aidha imeelezwa kuwa kuahirishwa kwa mashindano hayo kufanyika Malawi kumefuatia kutokea kwa machafuko ya Kisiasa na hii itatoa nafasi kwa mikoa iliyotajwa kuiona timu yao ya Taifa na baadhi ya wachezaji wakali wa mikoa hiyo kupata nafasi ya kucheza na wachezaji wa timu yhiyo ya Taifa.

Akizungumzia na mtandao huu kuhusu mashindano hayo, Katibu wa chama cha Pool Taifa. Amos Kafwinga alisema, ”Katika mashindano ya mwaka huu ya 'ALL AFRICA CUP –MALAWI' yamefutwa kutokana sababu zilizo nje ya uwezo wa chama cha pool Africa lakini tumefarijika sana kuona kwamba Bia ya Safari Lager bado iko na sisi bega kwa bega na kuipa nafasi timu yetu kufanya ziara ya michezo ya kirafiki na timu za mikoa’’ alisema katibu.

Akitoa salam za shukrani kwa Safari Lager kwa niaba ya Chama cha Mchezo wa Pool Tanzania (TAPA), Mwenyekiti wa chama hicho, Isaac Togocho alisema “ Tulipokea taarifa za kufutwa mashindano kwa masikitiko makubwa sana kwani tulikuwa tumejiandaa vilivyo kwa ajili ya mashindano hayo, lakini nilifarijika sana kusikia kuwa wadhamini wetu SAFARI LAGER wametupa nafasi ya kujiandaa zaidi kwa kutupa michezo ya kirafiki katika mikoa.

No comments:

Post a Comment