Wednesday, November 9, 2011

Wateja wa Airtel sasa kuupigia kura Mlima Kilimanjaro BURE


Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Airtel Tanzania, Beatrice Singano akiwa ameshikilia simu huku akitoa maelekezo namna ya kuupigia kura Mlima Kilimanjaro kura BURE kupitia Airtel ili uweze kuingia kwenye maajabu saba ya Dunia hadi tarehe 11 Novemba 2011.

******************************************

* Kilimanjaro kuwa moja kati ya maajabu 7 ya asili duniani
* Tuma sms nyingi uwezavyo bure

Kampuni ya simu za mkononi ya Airtel imeungana na serikali ofisi ya waziri mkuu pamoja na Bodi ya utalii Tanzania katika kuwezesha na kufanikisha kampeni ya kuupiga kura mlima Kilimanjaro kuwa kati ya maajabu saba ya dunia na kutoa nafasi kwa wateja wake nchi nzima kuweza kuupigia kura mlima wa Kilimanjaro bure.

Akiongea na waandishi wa habari mkurugenzi wa mawasiliano wa airtel Beatrice Singano Mallya alisema " Airtel Tanzania inadhamira ya kuchangia na kushirikiana na watanzania kote nchini kuhakikisha tunaendelea kuuweka Mlima Kilimanjaro katika historia ya Dunia na kua kati ya maajabu saba ya dunia.

"Mlima wa kilimajaro ni mlima mrefu kuliko yote Afrika na wa pili duniani na hivyo basi kuingia katika maajabu 7 ya dunia ni kitu cha kujivunia sio tu kwa watanzania bali Afrika nzima na marafiki wa Tanzania.

Katika kulitimiza hilo leo hii Airtel Tanzania inaatoa nafasi ya pekee kabisa kwa wateja wetu wote kuanza kupiga kura bure kupitia simu zao za airtel ili kuuongezea mlima wa Kilimanjaro nafasi kubwa zaidi ya kushinda.

Tupige kura kwa wingi tukizingatia pia taifa letu linatimiza miaka 50 ya uhuru, mafanikio ya kushinda itakua ni zawadi kwetu sote na jambo la kujivunia" alisema Mallya Jinsi ya kupiga kura, ni kwa kuandika ujumbe mfupi wenye neno KILI na kutuma kwenda 15771 kuanzia sasa, wajulishe na wengine wapige kura sasa ili kuuongezea Mlima wa Kilimanjaro nafasi ya kuwa katika maajabu 7."


Kwa niaba ya airtel Tanzania naomba watanzania wote tuchukue nafasi hii kutimiza dhamira yetu hii ambayo inafaida kwa taifa letu na Afrika kwa ujumla, mlima Kilimanjaro upo Tanzania lakini ni dhahiri kuwa sifa na faida yake hufaidisha nchi zote za Afrika.


Airtel tunawateja wa matabaka tofauti wanafunzi, wafanyabiashara, watumishi wa mashirika binafsi, watumishi wa mashirika ya umma na serikali sasa tunaomba tuwakumbushe kupiga kura kupitia airtel kwa sasa ni bure hivyo tunaomba wote watumie muda kidogo kwa kipindi hiki kupiga kura.

Airtel kupitia wafanyakazi wetu wote tayari tumeshaanza kupigakura na kuhamasisha kila mmoja kufanya hivyo na tunaamini pia wateja wetu watatuunga mkono katika kufanikisha jambo hili la kijamii.


Kwa upande wake meneja mahusiano wa Bodi ya Utlii Geofrey Tengeneza alisema,"Bodi ya utalii inatoa shukurani kwa Airtel kushirikiana nasi katika kuwezesha kampeni hizi, sisi kama Bodi ya utalii tunawataka watanzania sasa watumie fulsa hili ya lala salama kuweza kupigia kura kwa wingi mlima wetu ili uweze kuwa miongoni mwa maajabu hasa 7 mapya ya asili , kuna faida nyingi lakini kubwa zaidi ni kuongeza pato la taifa litokanalo na utalii.

Pamoja na sms tunaweza kupiga kura kwa kupitia tuvuti ambayo ni www.new7wonders.com Zimebaki siku tatu Ili kampeni ya kuuwezesha Milima Kilimanjaro kuingia katika orodha ya maajabu saba ya dunia kufikia ukingoni hivyo ni jukumu letu sisi watanzania kuupigia kura sasa.

No comments:

Post a Comment