Wednesday, January 25, 2012

DKT, WANYANCHA AENDELEA NA ZIARA YAKE YA KUKAGUA MADARJA- DSM


Mwenyekiti wa Bodi ya mfuko wa barabara (RFB) Dkt. James Wanyancha akiangalia mazingira ya eneo la mkondo wa mto unapita katika daraja la Kawe(kwa Malecela) Wilaya ya Kinondoni Jan, 23,2011 alipofanya ziara ya kukagua ukarabati wa ujenzi wa madaraja na makalavati ambapo mfuko wake umetoa fedha za kusaidia kukarabati, Vilevile ametoa wito kwa wakazi wanaoishi kandokando na madaraja kuwacha kutupa mataka (uchafu) na kuchimba mchanga baadae huasababisha kuharibu mazingira pamoja na mito kupoteza njia zake. (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
maenedeleo ya ukarabati wa eno la daraja la Matosa huko Goba katika wilaya ya Kinondoni mkoa wa Dar es Salaam ambalo Mwenyekiti wa Mfuko wa Bodi ya Barabara Dkt. James Wanyancha (hayupo pichani ) alikagua maendeleo ya ukarabati Jan, 23,2012, (Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Mwenyekiti wa Bodi ya RFB Dkt, James Wanyancha (kushoto) akisikiliza maelezo ya ukarabati kutoka kwa Mhandisi Julius Ngusa waTanroads Jan 23,2012 kuhusu maendeleo ya ukarabati wa daraja la eneo la Mbezi katika barabara iendayo Morogoro,ambayo iliharibiwa na mafuriko mwaka jana, (Picha na Mwanakombo Jumaa-MAELEZO).
Mwenyeki wa Mfuko wa Bodi ya Barabara James Wanyancha akitoa maelezo kwa waandishi wa habari pichani hawapo Jan, 23,2012 kuhusu maendeleo ya ukarabati wa eneo la daraja la Mbezi katika barabara ya Morogoro(Morogoro road (Mbezi) iliyoharibiwa na mafuriko ya mwaka jana,ambapo mfuko wake umetoa fedha za dharua zaidi ya shilingi bilioni tano(5b/-) zilizombwa za dharura na mkoa wa Dares salaam kwa ajili ya kusaidia ukarabati.(Picha na Mwanakombo Jumaa- MAELEZO).
Uharibifu wa mazingira kwenye daraja la boko watu wakiendelea kuchimba mchanga
Mafundi wakiendelelea na ukarabati huko barabara ya morogoro eneo la mbezi
Fundi akiwa kazini daraja la Salender Bridge

No comments:

Post a Comment