Thursday, January 12, 2012

SBL wakabidhi msaada wa flana Sherehe za Mapinduzi Zanzibar


Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akipokea msaada wa flana maalumu zitakazo tumika kwenye Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar zilizotolewa na Kampuni ya Bia ya Serengeti Breweries (SBL) kupitia kinywaji chake cha Malta Guinness leo, anayekabidhi ni Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda (kushoto) akizungumza kabla ya kukabidhi msaada wa flana 2000 zenye thamai ya sh milioni 15, anayesikiliza katikati ni Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd, kulia ni Waziri wa nchi Ofisi ya Makamu wa Pili wa Rais, Mohamed Aboud.
Mkurugenzi wa Mawasiliano wa Kampuni ya bia ya Serengeti Teddy Mapunda katikati akijadiliana jambo na meneja wa kinywaji cha Malta Guiness Maurice Njowoka, kushoto ni Meneja Mahusiano ya Jamii Nandi Mwiyombela.
Na Joachim Mushi, Zanzibar
KAMPUNI ya Bia ya Serengeti Breweries (SBL) kupita kinywaji chake kisicho na kilevi cha Malta Guinness wametoa msaada wa flana maalumu kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar (SMZ) zitakazotumika katika Maadhimisho ya Sherehe za Mapinduzi ya Zanzibar.
Akikabidhi flana hizo leo mjini Zanzibar Mkurugenzi wa Mawasiliano wa SBL, Teddy Mapunda kampuni hiyo imeamua kutoa msaada huo ikiwa ni mchango wao kushirikiana na SMZ kuadhimisha sherehe hizo za Mapinduzi.
Mapunda amesema SBL inaungana na SMZ pamoja na Wazanzibari wote katika kusherehekea siku kuu ya Mapinduzi, ambazo huadhimishwa kila ifikapo Januari 12, ya kila mwaka.
Amesema flana hizo 2,000 zinazogharimu sh. milioni 15 zitatumika katika maadhimisho ya sherehe hizo maalumu zinazofanyika kesho mjini hapa. SBL imesema itaendelea kushirikiana na SMZ katika masuala mbalimbali ya kijamii ikiwa ni ada ya kampuni hiyo ya kuisaidia jamii kupitia shughuli anuai za kijamii.
Naye Makamu wa Pili wa Rais wa Zanzibar, Balozi Seif Ali Idd akipokea msaada huo amsesema anaishukuru kampuni hiyo kwa msaada wao na kuiomba isiishie hapo katika kuisaidia Zanzibar.
“Tunawashukuru sana kwa flana hizi zitakazotumika sherehe za mapinduzi ya Zanzibar, lakini tunaomba msiishie hapo tuendelee kushirikiana na kusaidiana kwa mambo mengine pia,” alisema Balozi Idd.
Katika hafla hiyo fupi SBL pia iliwakilishwa na Meneja Uhusiano, Nandi Mwiyombela na Meneja wa kinywaji cha Malta, Maurice Njowoka.

No comments:

Post a Comment