Monday, January 9, 2012

TASWA FC YAFANYA MAUAJI YAICHAPA MUHIMBILI VETERAN'S 2-1


Beki wa timu ya Taswa FC, Ernest Mbozi (kulia) akimdhibiti mshambuliaji wa Muhimbili Veteran's, a.k.a (Watoto wa Islam Boban) Nsa Job, wakati wa mchezo wa kirafiki uliochezwa jana jioni kwenye Uwaja wa Muhimbili Hospitali. Katika Mchezo huo Taswa ilishinda mabao 2-1 na kufanya mchezo huo kuzua tafrani baada ya mchezaji aliyeachwa na kibao hata kwa mkopo wa 'Buku' Nsa Job, kuanza kucheza rafu ovyo na kuwaumiza wachezaji wa wawili wa Taswa, jambo ambalo lilisababisha vurugu kubwa uwanja ni hapo.
"Atakayenifuata tu nampa la uso" Kocha wa Taswa Fc, Aly Mkongwe, akiwa nje yauwanja wakati akitoa maelekezo kwa wachezaji watimu yake huku akijihami na silaha ya mawe, baadayamcezo huo 'kunuka' yaani kuharibiwa na mchezaji Nsa Job na kusababishavurugu. Picha ya chini Mchezaji wa Taswa Fc, Saleh Ally, akimpa maneno ya busara Nsa Job, baada ya kutaka kurusha ngumi kwa mchezaji wa Taswa, wakati aipocheza rafu mbaya na kumuumiza beki wa Taswa, Sweetbert Lukonge.
Na Mwandishi Wetu
TIMU ya soka ya waandishi wa habari za michezo nchini, Taswa FC imeanza mwaka kwa kishindo na kuvunja mwiko wa kutofungwa kwenye uwanja wa nyumbani wa timu ya Muhimbili Veterans baada ya kuichapa kwa mabao 2-1.
Mchezo huo uliofanyika Jumamosi jioni ulikuwa mkali na wa kusisimua kutokana na upinzani wa timu zotembili. Ikiongozwa na wachezaji wake nyota, Saleh Ally, Majuto Omary, Said Seif, Sweetbert Lukonge, Juma Ramadhani, Monishiwa Lihambiko, Mohamed Mharizo, Fred Mweta and Fred Mbembela, Taswa FC ilianza mchezo huo kwa kasi na kuzima kabisa cheche za wapinzani wao.
Muhimbili ambayo ilikuwa chini ya mchezaji nyota, Mussa Hassan Mgosi ambaye anachezea timu ya DC Motema Pembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo (DR Congo) na mchezaji aliyewahi kuchezea Simba, Yanga, Moro United, Azam FC na Vila Squad Nsa Job, walishindwa kuonyesha checeh zao kutokana na kufunikwa na wachezaji wenye vipaji wa Taswa FC.
Hali hiyo iliufanya mchezo huo kuwa na upinzani wa aina yake huku Taswa FC ikitawala muda mrefu na kipa wake, Shedrack Kilasi kuwa likizo muda wote. Baada ya kuwakosa kosa mara kibao, Taswa FC ilisheherekea bao lake la kwanza kupitia kwa Saleh Ali kufuatia ushirikiano mzuri baina yake na Said Seif, Majuto, Monishiwa na Mharizo.
Saleh alifunga bao hilo kwa ustadi mkubwa baada ya kumchungulia kipa wa Muhimbili Veterans kabla ya kufunga mithiri ya ‘kanzu’. Bao hilo liliwachanganya sana Muhimbili hasa baada ya mbinu zao zote za kutaka kusawazisha kuishia kwenye ukuta mkali wa Taswa FC.
Baada ya kuona wanashindwa, Muhimbili veterans wakiongozwa Nsa Job, kuanza kucheza rafu ambapo walifanikiwa kupunguza nguvu ya Taswa FC baada ya Job kumrukia guu mbili Lukongwe na kufanya kutibiwa kwa muda uwanjani hapo. Hata hivyo ukuta wa Taswa FC ulisimama imara na kuokoa hatari zote.
Kipindi cha pili kilianza kwa kila timukufanya mabadiliko ambapo Muhimbili ilibadili karibu asalimia 99 ya timu yake huku Taswa FC ikifanya mabadiliko kwa wachezaji wachache. Muhimbili ilisawazisha kupitia kwa Ali Mpemba, lakini bao lao halikudumu baada ya Taswa FC kushindilia msumali wa mwisho kupitia kwa Gilbert na kuacha kilio kwa wapinzani wao.

No comments:

Post a Comment