Sunday, February 12, 2012

HAFLA YA YANGA KUTIMIZA MIAKA 77 YAFANA PEACOCK HOTEL


Mdhamini wa timu ya Yanga ya Jangwani jijini Dar es salaam Mama Fatma Karume akizungumza katika hafla ya timu hiyo kuimiza miaka 77 tangu kuanzishwa kwake iliyofanyika jana kwenye hoteli ya Peacock na kuhudhuriwa na wanachama na wadau mbalimbali wa mpira wa miguu, huku mgeni rasmi akiwa Dk. Fenella Mkangara Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na michezo anayeonekana kulia katika picha kushoto ni baadhi ya wazee wa Yanga. Mama Fatma Karume alisema Yanga ni mzee wa miaka 77 lakini katika michezo anaweza kukimbia kwa kasi ileile ya kimichezo, hivyo akamuomba mola ili klabu hiyo izidi kupata mafanikio katika michezo.
Mgeni rasmi katika hafla ya timu ya Yanga kutimiza miaka 77 Dk Fenella Mkangara Naibu Waziri wa Habari, Vijana , Utamaduni na michezo akizungumza katika hafla hiyo, huku Mwenyekiti wa Yanga Loyd Nchunga akifurahia jambo, kulia ni Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sadik Meck Sadik na kushoto ni mdhamini wa Yanga Mama Fatma Karume.
Katibu Mkuu wa Yanga Selestini Mwesigwa akipiga mamombi kabla ya kuanza kwa hafla hiyo kulia ni George Kavishe Meneja wa kinywaji cha Kilimanjaro na kutoka kushoto ni Mwenyekiti wa Yanga Loyd Nchunga na Mkuu wa Mkoa wa Dar es salaam Sadik Meck Sadik.
Wadau kutoka Peacock Hotel wakijadiliana jambo ili kuhakikisha sherehe hiyo inafana zaidi.
Ancle Hashim Lundenga kulia ndani kama unavyomuona akiwa ametulia kitiniKutoka kulia ni Kocha mkuu wa Yanga Kostadin Papic shabiki mkubwa wa Yanga Emmanuel Mpangala na Kocha msaidizi wa timu hiyo mwenye (Mzuka Mwingi) Fred Felix Minziro wakifuatilia mambo mbalimbali katika hafla hiyo.
Kulia ni wanachama wa Yanga Mh. Mudhihir Mudhihir kulia na Jaji Mkwawa wakiwa katika hafla hiyo jana uziku.
Mashabiki ha wa pia walikuwepo kuipa tafu klabu yao.
Kundi la THT likitumbuiza katika hafla hiyo
Hii ndiyo mandhari ya ukumbi inavyoonekana katika picha

No comments:

Post a Comment