Monday, February 13, 2012

KAMISHENI YA NGUMI ZA KULIPWA NCHINI TPBC YAFANYA MABADILIKO KIUTENDAJI

Hivi karibuni kumekuwepo na ulazima wa mabadiliko katika Kamisheni ya Ngumi za Kulipwa nchini (TPBC) yanayotokana na changamoto zifuatazo:

1. Kuajiriwa kwa Boniface Wambura aliyekuwa Msemaji wa TPBC kuwa Msemaji

wa TFF. Wambura amefanya kazi nzuri sana tangu achukue jukumu la kuwa

Msemaji wa TPBC na ndiko alikoonekana kwa kazi nzuri na kuajiriwa TFF. Lakini

kwa kutambua kuwa kunaweza kuwa na mgongano wa maslahi, tumelazimika

kumpunguzia majukumu yake ili aweze kufanya kazi yake kwa ufanisi zaidi TFF.

Tunasikitika kumwachia mtendaji mzuri huyu! Msemaji wa Kamisheni sasa

atakuwa Rais wa Kamisheni Onesmo Ngowi.
2. Ukuaji wa mtandao wa ngumi kitaifa na kimataifa3. Matatizo kadhaa wa kadha katika medani ya ngumi za kulipwa Ili kukabiliana na changamoto zilizotajwa hapo juu, TPBC ilimteua Godfrey Madaraka Nyerere kuwa Makamu wa Rais December mwaka jana. Pia kitengo cha Fedha na Mipango kitakuwa chini ya makamu wa Rais. Uteuzi wa Madaraka ulifuatia mchango wake mkubwa kwenye medani ya ngumi za kulipwa kama Kromota, Kamaisha wa TPBC kanda ya Ziwa na Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TPBC kwa kipindi kirefu. Pamoja na mabadiko haya, TPBC inaendelea kifanya mabadiliko yafuatayo kwa kuunda Kanda Mpya ya Ngumi za Kulipwa ya Dar-Es-Salaam na kumteua bondia wa siku nyingi na bingwa wa kwanza wa dunia toka Tanzania Rashid "Snake Boy” Matumla kuwa Kamishna wa Kanda Mpya ya Dar-ES-Salaam. Aidha, TPBC imeunda Kamati zifuatazo:


Kamati ya Viwango na kumteua Boniface Wambura kuwa Mwenyekiti wake.


Kamati ya Ubingwa na kumteua John Chagu kuwa Mwenyekiti wake. Chagu amekuwa Referii na jaji wa ngumi za kulipwa wa siku nyingi anayetambuliwa na mashirikisho mengi ya ngumi duniani kama vile IBF. WBC, WBA na WBO.



TPBC imeteua Makamishna wa Kanda kama ifuatavyo:1. Kanda ya Dar-Es-Salaam: Rashid “Snake Boy” Matumla
2. Kanda ya Kaskazini: Mh. Justine Nyari
3. Kanda ya Kusini: Nicholas Mallya



Justine Nyari ni Diwani wa Mererani kwa tiketi ya CCM na ni mtu aliyefanya kazi na TPBC katika miaka ya nyuma na anapenda kusaidia maendeleo ya ngumi nchini.



TPBC imeteua pia Makamishna wa baadhi ya Mikoa kama ifuatavyo:
1. Mkoa Dar-Es-Salaam: Issa Maranga 2. Mkoa wa Tanga: Ibra Steke 3. Mkoa wa Kilimanjaro: Henry Mfinanga 4. Mkoa wa Arusha: Roman Chuwa
5. Mkoa wa Morogoro: Rauriti Bazi


Issa Maranga mwalimu wa shule ya St. Anthony na mpenzi wa ngumi wa muda mrefu.

Abra Steke ni bondia wa muda mrefu na mfanyakazi wa benki ya CRDB Tanga.

Henry Mfinanga ni mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya TPBC na ni mfanyabishara. Roman Chuwa ni mfanyabishara wa Utalii mjini Arusha na mpenzi na mfadhili wa TPBC. Rauruti Bazi anafanya kazi Kampuni ya Tumbaku na amekuwa mpenzi na mfadhili wa TPBC kwa muda mrefu.



Tutaendelea kufanya mabadiliko jinsi siku zinavyokwenda ili kufikia malengo ya Mpango Mkakati wa TPBC 2012 - 2013 wa kuleta maendeleo ya Ngumi hapa Tanzania.


Aidha, TPBC imetoa vibali kwa mabondia Francis Miyeyusho na Fadhili Majia kucheza ngumi nchini Uingereza mwanzoni mwa mwezi wa tatu katika mapambano yasiyo ya ubingwa.


Francis Miyeyusho atapambana 17 March katika ukumbi wa Sheffield katika jiji la London, ambapo bondia Fadhili Majia atapambana na Ashye Sexton tarehe 2 March Sheffield pia katika jiji la London.
Imetolewa naOnesmo A.M.NgowiIBF/USBA President for Africa
Director, Commonwealth (British Empire) Boxing Council (CBC)
President, Tanzania Professional Boxing Commission (TPBC)Tel: 0754-360828

No comments:

Post a Comment