Monday, February 20, 2012

MABONDIA SALEHE MKALEKWA NA ABDALAH MOHAMED (PRINCE NASEM) WATAMBIANA








Bondia Salehe Mkalekwa (kushoto) na Abdalah Mohamed (Prince Nasem) wakitunishiana misuri Dar es salaam jana wakati wa kutambulisha mpambano wao wa ubingwa wa KG 67 Watel weight litakalofanyika feb 24.katikati ni mratibu wa mpambano huo Shabani Adiosi (Mwaya Mwaya)




BINGWA wa mkanda wa Shirikisho la ngumi za kulipwa Tanzania (PST) Abdalah Mohamed 'Prenc Naseem' atapanda ulingoni kutetea mkanda wake wa PST Februari 24 mwaka huu dhidi ya Salehe Mkalekwa

Pambano hilo la ubingwa wa PST litakuwa ni pambano la uzito wa kg 67 na litashirikisha mapambano mengine manne ya utangulizi.

Akizungumza Dar es Salaam jana, Mratibu wa pambano hilo Shaban Adiosi 'Mwayamwaya' alisema pambano hilo litafanyika katika ukumbi wa New Kibeta uliopo mbagala kuu Dar es Salaam.

Alisema pambano hilo la ubingwa wa PST ni muendelezo wa shirikisho hilo kuendelea kuinua mabondia ambao hawajawa na majina makubwa ili nao waweze kufikia kiwango kizuri cha mchezo huo.

"Ubingwa huu wa PST ni maalum kwa ajili ya mabondia chipkizi na ndio maana mabondia wanaoshirikishwa wengi ni chipkizi na lengo ni kuendeleza vipaji vyao,"alisema Mwayamwaya.

Aliyataja mapambano ya utangulizi yatakayopamba pambano hilo yatakuwa kati ya Shaaban Zungu na Hasan Debe watakaopigana uzito wa kg 55,Safari Mbeyu na Ibrahim Maokola watakaopigana uzito wa kg 67, Jofrey Pacho atakayetwangana na Dickson Kawiani na Kulwa Kindondi atakayepigana na Khaji Hamisi.

Mbali na kuwepo mapambano ya ngumi kutakuwa na uuzwaji wa DVD zenye mapambano ya mabingwa wa Dunia akiwemo Manny Paquaio, Floyd Maywherth, Roy Jones, Lenox Lewis,David Haye na wengine kibao ‘DVD’ hizo zilizoandaliwa kwa ubora wa hali ya juu zitakuwa zikiuzwa kwenye mpambano huo na Kocha wa Kimataifa wa Mchezo wa Ngumi, Rajabu Mhamila ‘Super ‘D’.

“Ninatarajia kuwapelekea DVD mashabiki wa ngumi watakaokuwepo katika pambano kujifunza mambo mbalimbali ikiwa ni pamoja na sheria za mchezo wa ngumi,” alisema Super ‘D’.

No comments:

Post a Comment