Saturday, February 25, 2012

MAMA ASHA BILAL ATEMBELEA KITUO CHA WATOTO YATIMA CHA KATANDALA SUMBAWANGA







Mke Wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akisalimiana na mmoja kati ya watoto Yatima, Juma, baada ya kuwasili kwenye Kituo cha kulelea watoto Yatima cha Katandala kilichopo Sumbawanga jana Februari 24, 2012 kwa ajili ya kukabidhi Tanki la kuhifadhia maji la Lita 5000 katika kituo hicho. Picha na Muhidin Sufiani-OMR


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akisalimiana na mfanyakazi wa kujitolea kutoka nchini Ujerumani, Liza Gernemann, aliyembeba mtoto William wa Kituo cha kulelea Watoto Yatima cha Katandala, wakati alipofika katika kituo hicho jana Februari 24, 2012 kwa ajili ya kukabidhi Tanki la kuhifadhia maji la Lita 5000. Picha na Muhidin Sufiani-OMR


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, akiwa amembea mmoja kati ya watoto Yatima wanaolelewa katika Kituo cha kulelea watoto hao katika Kituo cha Katandala, wakati akitembelea katika vyumba vya kulala vya watoto hao, alipofika kukabidhi Tanki la maji la Lita 5000 kituoni hapo jana Februari 24, 2012. Kushoto kwake ni Mkuu wa Mkoa wa Sumbawanga na Katavi, Eng. Stella Manyanya. Picha na Muhidin Sufiani-OMR


Mke wa Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mama Asha Bilal, kishikana mkono na Mkuu wa Kituo cha kulelea watoto Yatima cha Katandala, Sr. Maria Goreth Chusu, ikiwa ni ishara ya kumkabidhi Tanki la kuhifadhia maji la Lita 5000 katika kituo hicho alipofika kituoni hapo kilichopo Sumbawanga jana Februari 24, 2012. Kushoto kwa Mama Asha ni Mkuu wa Mkoa wa Sumbawanga na Katavi, Eng. Stella Manyanya (kushoto) ni Sr. Scolastica Mwembezi. Picha na Muhidin Sufiani-OMR


No comments:

Post a Comment