Thursday, February 16, 2012

Mkuu wa wilaya Mkuranga awafagilia SHIWATA





Na Mwandishi Wetu, Mkuranga MKUU wa Wilaya ya Mkuranga,Henry Clemence amewataka wanachama wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA) kuchangamkia ujenzi wa nyumba zao katika kijiji cha Mwanzega Kimbili wilayani humo kwa sababu ni eneo linaloweza kubadilisha maisha yao kwa haraka. Akizungumza wakati akimkaribisha Mwakilishi wa Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Mkurugenzi wa Utamaduni wa wizara hiyo Profesa Herman Mwansoko na uongozi wa SHIWATA ofisini kwake juzi alisema wasanii wanatakiwa kuenziwa kwa kazi kubwa wanayoifanya ya kuonya, kuburudisha na kufundisha kupitia sanaa lakini kipato chao ni duni. Mkuu huyo wa wilaya alisema SHIWATA walipofika kuomba viwanja vya ujenzi aliwakaribisha na kuwapa msaada huo akijua kuwa wasanii wana wajibu mkubwa katika jamii lakini thamani ya kazi zao haziwasadii kupata maisha bora. "Wasanii walipofika kuomba eneo la kujenga nyumba za kuishi, sikusita kuwapokea, mimi najua mchango wa sanaa katika jamii, nawahakikishia kuwa Mkuranga ni eneo lenye rutuba kwa kipindi chote cha mwaka, mtalima na kuzalisha mazao ya kuwasaidia katika maisha yenu" alisema Mkuu wa wilaya Clemence. Mwakilishi wa Waziri Emmanuel Nchimbi, Mkurugenzi wa Utamaduni, Mwansoko wakati akikagua nyumba tano zilizojengwa na wasanii kwa njia ya kuchangishana kwa thamani ya sh. mil. 33,000 alisema wizara yake imeunda kuunda Kamati ya filamu na muziki ili kutatua migogoro ya mara kwa mara inayojitokeza katika fani hizo. Alisema kabla ya hamasa ya wasanii kutafuta eneo la ujenzi, Wizara ilikutana na wasanii wote nchini na kutafakari jinsi watakavyoweza jkuungana kujikwamua kiuchumi. Aliwataka wasanii kutumia eneo walilopewa na wilaya ya Mkuranga kutenga eneo la kujenga sehemu za kujifunza sanaa eneo hilo la makazi. Mwenyekiti wa Bodi ya Filamu Tanzania, Bibi Rose Sayore alisema tukio na wasanii kujenga nyumba hizo ni ukombozi ambao watanzania walitaka kuona inafanyika kwa sanii Tanzania. Mwenyekiti wa SHIWATA, Cassim Taalib alisema wametenga maeneo ya kujenga kumbi za kufanyia mazoezi na kutenga maeneo ya kujenga huduma za Zahanati, shule na nyumba za kuabudia. Shekhe Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Shekhe Alhad Mussa Salum aliyefuatana na msafara huo alisema kuna taasisi ya kiislamu imejitokeza kuchimba visima vya maji katika kijiji cha Mwanzega, Kimbili. Naye Ofisa Tawala wa Mkuranga, Bi. Joyce Nampesya amewataka wasanii wasiishie ujenzi wa nyumba tano walizojenga kubaki kuwa shoo na mradi kuishia hapo bali amewataka waongeze juhudi za kuwajengea wasanii wote wanachama

No comments:

Post a Comment