Saturday, February 18, 2012

RAIS JAKAYA KIKWETE ASHIRIKI MATEMBEZI YA KUCHANGISHA FEDHA KUSAIDIA KINA MAMA WENYE MATATIZO YA FISTULA





Rais Jakaya Kikwete wa nne kutoka (kulia) akishiriki katika matembezi ya kuchangia shilingi Bilioni moja kwa ajili ya ujenzi wa jengo la akina mama wenye matatizo ya ugonjwa wa Fistula katika hospitali ya CCBRT leo asubuhi jijini Dar es salaam, matembezi hayo yameanzia katika hoteli ya Golden Tulip na kumalizika katika Hospitali ya CCBRT Mikocheni, matembezi hayo yameandaliwa kwa pamoja na kampuni ya Vodacom Tanzania, Vodafone pamoja na hospitali ya CCBRT Kampeni hiyo inajulikana kama (Finde your Moyo).


Katika picha kutoka kulia ni Erwin Telemans Mkurugenzi mtendaji wa CCBRT, Rene Meza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania, Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya CCBRT Bw. Wilbroad Slaa na kushoto kwa Rais ni Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dr. Hadji Mponda wakishiriki katika matembezi hayo leo asubuhi.


Rais Jakaya Kikwete akizungumza na Mkurugenzi wa Huduma za Jamii wa CCBRT, Brenda Msangi katikati alipokuwa akipata maelezo mbalimbali wakati alipowasili katika hospitali hiyo baada ya matembezi hayo, kushoto ni Dk. Brenda kutoka hospitali ya CCBRT.

Rene Meza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania akitoa hotuba yake kabla ya kuanza kwa matembezi hayo leo asubuhi.

Watu mbalimbali waliojitokeza katika matembezi hayo wakiwa katika hoteli ya Golden Tulip leo asubuhi.

Mwenyekiti wa Bodi ya wakurugenzi ya CCBRT Bw. Wilbroad Slaa akizungumza na Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba.

Ofisa Mkuu wa Masoko na Mahusiano wa Vodacom Tanzania Mwamvita Makamba akizungumza na Rene Meza Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania.

Wakiwa katika mzungumzo kabla ya kuanza kwa matembezi hayo kulia ni Kamanda wa Kanda Maalum ya Dar es salaam ya kipolizi Suleiman Kova, Mkuu wa Wilaya ya Kinondoni Jordan Rugimbana na Waziri wa Afya na Ustawi wa Jamii Dk. Hadji Mponda.

Mkurugenzi wa Kurugenzi ya Mawasiliano Ikulu Salva Rweyemamu akijadili jambo na Meneja Udhamini na Matukio wa Vodacom Tanzania Rukia Mtingwa.

Watu mbalimbali walioshiriki katika matembezi hayo

Kulia ni Grace Lyon wa Vodacom Tanzania, Meneja wa Vodacom Foundation Yesaya Mwakifulefule na Matina Nkurlu Meneja wa kitengo cha habari za Mtandao Vodacom Tanzania.

Wadau wangu wakubwa kulia ni Bw. Philip Seyayi aka (Shvangirai) kutoka JWT na Ofisa Udhamini wa Vodacom Tanzania Ibrahim Kaude wakipata viroba vyao! Ah ni utani tu jamani hii ni Juice.

No comments:

Post a Comment