Monday, February 27, 2012

TRA YAANZISHA MPANGO MPYA WA UKUSANYAJI KODI





NA GLADNESS MUSHI WA FULLSHANGWE- ARUSHA

MAMLAKA ya mapato Tanzania(TRA)imeanzisha utaratibu wa ukusanyaji

kodi shirikishi kwa kutoa elimu ya mlipa kodi kwa wafanyabiashara nchi nzima,ikiwa ni mkakati wa kuongeza mapato ya serikali bila shuruti

Aidha mkakati huo ambao umeanzia katika mikoa ya kanda ya kaskazini,unalenga kuwafanya wafanyabiashara waelewe kuwa TRA ni rafiki ya mlipa kodi na kwamba kulipakodi bila shuruti ni wajibu kwa maendeleo ya taifa. Meneja wa mambo ya ndani ,ofisi ya kamishina mkuu wa TRAnchini,Bi Stela Cosmas aliyasema hayo wakati alipokuwa akizungumza na chama cha wafanyabiashara mkoani Arusha(TCCIA)

Cosmas aliwataka wafanyabiashara kufuata taratibu nakanuni za mlipa kodi ikiwemo kutoa stakabadhi zilizosahihi kwa wateja wao kuwasilishamalipo ya kodi sahihi,ritani sahihi, nyaraka za forodha na madai ya marejesho ,kutoa na kudai stakabadhi ankra za kodi .Aidha alito wito kwa wafanyabiashara kuepuka ukwepajikodi kwa kutumia risiti,ambapo alidai yakuwa wafanyabiashara wamekuwa na tabiaya kumwandikia mteja risiti yenyekiwango tofauti na iliyopo kwenye kitabu chake cha mauzo,kwani kwa kufanyahivyo ni kuinyima serikali mapato na ninikinyume cha sheria. Kwa upande wake meneja wa mamlaka ya mapato mkoa wa Arusha,EvaristKileva alisema kuwa, wajibu wao kama TRA ni kuhakikisha kuwa wanahamasisha walipa kodi kulipa kodi kwa wakati kwa ajili ya manufaa ya watanzania kwa ujumla . Kileva alisema kuwa wadau wakuu wa TRA ambao niwalipa kodi wanapaswa kuhudumiwa kwa umakini mkubwa bila kuwepo kwa malalamikoyoyote kati yao na mamlaka husika ambapo alisema endapo kutakuwepo na kutokuelewanakati yao na wafanyakazi wa TRA wawakilishe malalamiko yao kwa meneja mwenyeweili yaweze kuchukuliwa hatua. Aliongea kuwa, ni vizuri walipa kodi wakawa na mahusianomazuri kati yao na mamlaka ya mapato ili kuboresha huduma zinazotolewa bilakuwepo kwa vikwazo vya aina yoyote ikiwa ni pamoja na walipa kodi kujijengea tabia ya kuwasilisha malalamiko kwa wakati na kwa mamlaka hiyo na sio nje yahapo huku lengo hasa likiwa ni kuendelea kudumisha mahusiano mazuri . ‘’ndugu zanguwafanyabiashara ofisi yetu ipo wazi kila siku kwa ajili yenu tafadhili kamakuna matatizo yanajitokeza msikumbatie malalamiko leteni ofisini’’alisema Bw Kileva Alisema kuwa, elimu hiyo imeweza kuwanufaisha kwa kiasikikubwa sana kwani hapo awali walikuwa hawana uelewa wowote jinsi ya kuwahojiwatendaji wa TRA pindi wanapofika katika maeneo yao kwa ajili ya kudai kodi Alifafanua kuwa kupitia mafunzo hayo yamewawezesha kwakiasi kikubwa sana kuwa na mahusiano mazuri kati yao na mamlaka hiyo ,pamoja nawatendaji wa mamlaka kwa ujumla kwani wataweza kufanya kazi kwa ushirikiano wahali ya juu tofauti na ilivyokuwa hapo awali.

No comments:

Post a Comment